Connect with us

General News

Karua aanza kumpigia debe Raila Kirinyaga – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Karua aanza kumpigia debe Raila Kirinyaga – Taifa Leo

Karua aanza kumpigia debe Raila Kirinyaga

NA GEORGE MUNENE

KIONGOZI wa Narc Kenya, Martha Karua amezindua kampeni za Azimio One Kenya Alliance katika Kaunti ya Kirinyaga na kuapa kumpigia debe mgombeaji urais, Raila Odinga.

Katika hafla iliyofanyika Ijumaa kwenye hoteli ya Starwood, mjini Kerugoya, Bi Karua alifafanua kuwa anamuunga mkono Bw Odinga kutokana na ajenda zake kumi. “Ajenda yake inagusia kuhusu afya na inapaswa kukumbatiwa na Wakenya wote,” alisema.

Aliwapuuzilia mbali wanaomshambulia kwa kujiunga na muungano wa Azimio. “Nilitathmini miungano yote ya kisiasa nikachagua Azimio kwa sababu ninaamini ndiyo bora,” alisema.

Aliapa kufanya kazi na viongozi maarufu watakaohakikisha fedha za umma zinalindwa.

Bi Karua aliwaeleza viongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza kukoma kuwatusi wapinzani wao wanapokuwa kwenye kampeni za kisiasa.

Alisema viongozi hao wanapaswa kujiepusha na matusi ikiwa wanataka kuheshimiwa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending