Connect with us

General News

Karua ajiunga na OKA akiahidi kutumikia nchi vyema wakishinda urais – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Karua ajiunga na OKA akiahidi kutumikia nchi vyema wakishinda urais – Taifa Leo

Karua ajiunga na OKA akiahidi kutumikia nchi vyema wakishinda urais

Na PIUS MAUNDU

SIKU chache tu baada ya Musalia Mudavadi (ANC) na Moses Wetang’ula (Ford Kenya) kuhama OKA, Muungano huo umepigwa jeki baada ya Kinara wa Narc Kenya kujiunga nao rasmi Jumamosi.

Bi Karua jana Jumamosi alihudhuria mkutano wa viongozi wa OKA katika uwanja wa Mulu Mutisya, Kaunti ya Machakos alikosema ujio wake ulikuwa wa kudhihirisha wako pamoja katika safari ya kuhakikisha Kenya inapata uongozi bora.

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, Mwenyekiti wa Kanu Gideon Moi na wanasiasa kadhaa kutoka kaunti tatu za Ukambani pia walihudhuria mkutano huo.

“Tuko hapa kuwadhihirishia kuwa sote tumejumuika pamoja hadi wakati wa mwisho. Tutawafanyia kazi kama watumishi wenu wala si mabosi,” akasema Bi Karua akishangiliwa na umati uliokuwa uwanjani humo.

Bi Karua sasa anapandisha hadhi OKA inayoonekana kama muungano unaoweza kuzuia kiongozi wa ODM Raila Odinga na Naibu Rais William kupata ushindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Bi Karua amekuwa akiongoza vuguvugu la Umoja wa Mlima Kenya (MKUF).

Bi Karua analenga kiti cha ugavana wa kaunti ya Kirinyaga.

Katika mkutano wa Jumamosi, Bw Musyoka kwa mara nyingine aliendelea kumkashifu Bw Mudavadi, akisema kuwa heri angesalia OKA ambako alikuwa ameahidiwa wadhifa wa Naibu Rais kuliko kambi ya Ruto ambapo hatapata chochote.

Bw Musyoka pia alikariri kuwa hatashawishiwa kujiunga na mrengo wa Bw Odinga huku Bw Moi akisisitiza OKA iko imara na itakuwa katika serikali ijayo.