Connect with us

General News

Karura Greens yapania kushiriki ngarambe ya CAF katika siku za usoni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Karura Greens yapania kushiriki ngarambe ya CAF katika siku za usoni – Taifa Leo

Karura Greens yapania kushiriki ngarambe ya CAF katika siku za usoni

NA JOHN KIMWERE

KLABU ya Karura Greens FC ni kati ya vikosi vinavyopania kupambana mwanzo mwisho kwenye kampeni za kufukuzia ubingwa wa taji la Nairobi West Regional League (NWRL) muhula huu.

Karura Greens imeorodheshwa miongoni mwa washiriki wa Kundi B kupigania ubingwa wa kipute hicho msimu huu.

Karura Greens ambayo hupatikana eneo la Gachie, Kiambaa, Kaunti ya Kiambu ndio mara ya pili kushiriki mechi za kinyang’anyiro hicho.

”Tunafahamu hakuna kitu kizuri kinachopatikana bila jasho na ndiyo maana tunajituma kwa udi na uvumba kupigania tiketi ya kupandishwa ngazi msimu ujao,” mwenyekiti wake, Duncan Dawa alisema na kuongeza kuwa muhula huu wamepania kujituma kwa udi na uvumba wanakolenga kuibuka nafasi ya kwanza na kusonga mbele baada ya kumaliza nne bora msimu uliopita.

Mchezaji wa timu ya Karura Greens FC (manjano) akikwepa wachezaji wa timu pinzani wakati wa mechi ya awali ya kipute cha Nairobi West Regional League (NWRL). PICHA | JOHN KIMWERE

Mwenyekiti huyo anazidi kusema kuwa vijana wake wamekaa vizuri kuonyesha weledi wao kwenye kampeni za muhula huu na kufanya kweli.

”Ufanisi wetu kwenye mechi za kipute cha msimu uliyopita unaashiria wazi kuwa raundi hii tukiendeleza tulipoachia tutafinya wapinzani wetu na kubeba tiketi ya kusonga mbele,” akasema.

Kubuniwa

Patroni wa klabu hii, Donvin Oguda anasema ilianzishwa mwaka 2013.

”Tangia tuanzishe timu hii mwaka 2013 licha ya changamoto za kifedha tunazozidi kukubana nazo tunaendelea kuonyesha dalili za kufanya kweli katika soka la hapa Kenya,” akasema Oguda.

Naye Kocha mkuu, Robert Opon anadokeza kuwa wanajipatia miaka mitano pekee kuhakikisha wamefuzu kushiriki Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF-PL). Aidha anasema kuwa wanatamana sana miaka ijayo kufuzu kushiriki mashindano ya mabingwa wa Ligi Kuu katika mataifa ya Afrika (CAF).

”Ili kutimiza maazimio mengine kama kushiriki kati ya vipute vya haiba kubwa Afrika hakika tunahitaji ufadhili mzuri kwa ajili ya kusaini wanasoka bora na kuwalipa ujira mzuri,” kocha huyo alisema na kutoa wito kwa wahisani wajitokeze na kuwaungana mkono ili kuipasha mchezo huo kwa wachana nyavu wanaokuja nchini.

Sajili wapya

Kwenye maandalizi ya kushiriki ngarambe ya msimu huu, Karura Greens ilisaini wachezaji wawili kujiongezea nguvu akiwamo Hillary Agesa (Makarios 111 Riruta United) na Jimmy Wafula (Kibra United).

Kwenye kampeni za kipute hicho naibu kocha, Kennedy Odiwuory anasema, ”Katika mpango mzima tumepania kujituma kisabuni ili kutwaa ubingwa wa mechi za muhula huu lakini tunafahamu tunatarajia upinzani wa kufa mtu.”

Kocha huyo alitaja baadhi ya vikosi vinavyowatoa kijasho kama Red Carpet, Shofco Mathare na Maroon Young Stars kati ya nyingine.

Karura Greens imeundwa na: Emmanuel Miheso, Hillary ‘Agu’ Agesa, Brian Kazungu, Edwin Otieno, Dennis Shisanya(naibu nahodha), Josphat Ngojo, Ochieng Boaz, Francis Kavithi, Kevin Ochieng, Alex Kamau, Gabriel Handache na Kennedy Juma (nahodha). Pia wapo Clinton Kanda, Peter Odhiambo, Jimmy Wafula, Theopholes Magina, Gideon Maina, Philip Osundwa, Joseph Otieno, Thomas Odera na Richard Mulandi.

Pandashuka

Karura Greens kama ilivyo kwa klabu zingine inapitia changamoto kibao hasa kukosa ufadhili. Moafisa wake wanasema kuwa hutumia michango kutoka kwa wafuasi wao ambayo kamwe haitoshi mboga kugharamia mahitaji yao michezoni.

”Itakuwa furaha kwetu endapo tutafanikiwa kupata wadhamini kutupiga jeki kwenye juhudi zetu michezoni,” Patroni huyo alisema na kuongeza kuwa usafiri kushiriki mechi za ugenini huwa tatizo kwao pia vifaa vya kuchezea bila kuweka katika kaburi la sahau dawa za kutoa huduma ya kwanza kwa wachezaji wanapopata majeraha wakicheza.