[ad_1]
Kaunti kusaidia wagonjwa kupokea huduma
NA KALUME KAZUNGU
SERIKALI ya Kaunti ya Lamu, imeamua kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba wagonjwa wote wanaohitaji kuhudumiwa mara kwa mara, hawatatatizika siku za usoni, jinsi ilivyoshuhudiwa wakati wa janga la virusi vya corona.
Ripoti ya utafiti wa idara ya afya katika kaunti hiyo imeonyesha kuwa, wagonjwa wa sukari na shinikizo la damu ndio walitatizika zaidi kupokea huduma za matibabu katika kipindi hicho.
Ripoti hiyo ya kutathmini huduma ya hospitali na vituo vya afya katika Kaunti ya Lamu, imeonyesha kuwa wengi wa wagonjwa hao walishindwa kufuatilia matibabu yao wakihofia maambukizi ya Covid-19.
Waziri wa Afya katika kaunti hiyo, Bi Anne Gathoni, pia alifichua kuwa kiwango cha chanjo za kinga ya maradhi kwa watoto kilishuka pakubwa wakati wa janga hilo.
Bi Gathoni alisema changamoto zilitokana na matangazo ya Wizara ya Afya kwamba watu wasalie nyumbani kuepuka kuambukizwa Covid-19.
Kulingana naye, kina mama wajawazito na watoto pia walikwepa kabisa huduma za chanjo zinazohitajika za kuwakinga dhidi ya maradhi kwani hawakutaka kutemebelea mazingira yoyote ya hospitali kutokana wakihofia kuambukizwa Corona.
Waziri huyo aidha alishikilia kuwa maradhi kama vile sukari na shinikizo la damu bado ni tatizo sugu hasa kwa wazee wengi kote Lamu, hivyo akawahimiza wananchi kuzingatia lishe bora, kuepuka ulaji mbaya na kufanya mazoezi ya mwili ili kuepuka kuugua maradhi hayo.
Next article
Kivumbi ndani ya Azimio jijini
[ad_2]
Source link