Connect with us

General News

Kaunti ya Kwale yalenga kuendeleza rekodi nzuri ya kuzuia udanganyifu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kaunti ya Kwale yalenga kuendeleza rekodi nzuri ya kuzuia udanganyifu – Taifa Leo

KCSE 2021: Kaunti ya Kwale yalenga kuendeleza rekodi nzuri ya kuzuia udanganyifu

NA SIAGO CECE

WATAHINIWA 831,015 wa Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) wameanza kuufanya kote nchini leo Jumatatu, Machi 14, 2022.

Mkurugenzi wa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) Kaunti ya Kwale Elias Gitonga amesifu kaunti hiyo akisema kwa miaka mitano mfululizo hakujaripotiwa kisa cha udanganyifu.

Amesema anatarajia kila kitu kuwa shwari mwaka huu kuendeleza rekodi hiyo nzuri.

Naye Afisa wa TSC Bi Perpetua Wairimu akihutubu katika Kaunti ya Kwale amesema mtihani huo utakamilika Aprili 1, 2022.

Afisa wa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) Perpetua Ngugi (kulia) akipeana karatasi za mitihani kwa mwalimu mkuu katika afisi za Kwale, Machi 14, 2022. PICHA | SIAGO CECE

Ameelezea matumaini yake kwamba hakutakuwa na udanganyifu katika KCSE.

Aidha, Wizara ya Elimu imeweka mikakati ya kutosha kuhakikisha walimu na maafisa wengine muhimu wanaosimamia mtihani huo hawatembei kwa muda mrefu kupeleka karatasi za mtihani kwa watahiniwa katika vituo mbalimbali.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending