Connect with us

General News

Kaunti yajitetea kuhusu usafiri uliomeza Sh410m – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kaunti yajitetea kuhusu usafiri uliomeza Sh410m – Taifa Leo

Kaunti yajitetea kuhusu usafiri uliomeza Sh410m

Na STEPHEN ODUOR>>

SERIKALI ya Kaunti ya Tana River, imejitetea kuhusu ripoti ya mhasibu wa fedha za taifa iliyoonyesha kuwa Sh410 milioni zilitumiwa kwa usafiri wakati wa janga la corona.

Kulingana na ripoti hiyo, kaunti hiyo inayoongozwa na Gavana Dhadho Godhana ilitumia pesa hizo kwa usafiri ilhali kulikuwa na masharti ya kuzuia usafiri.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha katika Kaunti, Bw Matheew Babwoya, alisema afisi ya gavana haifai kulaumiwa kikamilifu kwani Sh253 milioni zilitumiwa na bunge la kaunti.Hata hivyo, aliongeza kuwa kiasi kikubwa kilikuwa cha kulipia ada za awali za usafiri ambazo zilikuwa hazijalipwa katika kipindi cha kifedha kilichotangulia.

Wanaharakati walikuwa wameishinikiza kaunti hiyo ieleze jinsi fedha hizo zilitumiwa, kwani wakati huo mikutano mingi ilikuwa ikifanywa mitandaoni ili kuepusha mtagusano.