Connect with us

General News

Ken Mijungu miongoni mwa wafanyikazi waliofutwa kazi Nation Media

Published

on

Siku chache baada ya kampuni ya Nation Media Group kutangaza kupunguza idadi ya wafanyikazi kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, leo, Ijumaa, Julai 3 shoka hilo limeanza kuwaangukia baadhi yao.

Mtangazaji Ken Mijungu ni mmoja wa wafanyikazi ambao wamepigwa kalamu kutoka kampuni hiyo ambayo amehudumu kwa miaka saba.

Ken Mijungu afutwa kazi NTV baada ya kuhudumu kwa miaka 7

Ken Mijungu afutwa kazi NTV baada ya kuhudumu kwa miaka 7

Ken Mijungu alithibitisha haya kwenye ujumbe aliouchapisha mtandaoni na kusema alikuwa amepokea barua ya kumfuta kazi tayari.

“Shoka lilianguka katika chumba cha habari NTV na mimi ni mmoja wa walioangukiwa. Nilipokea barua ya kufutwa kazi baada ya kuhudumu kwa miaka saba,” mtangazaji huyo alisema.

Kwenye ujumbe huo alimshukuru Mungu kwa fursa aliyompa na vile vile mashabiki.

“Safari ingalipo. Namshukuru Mungu, atasalia kuwa mkuu, nashukuru kwa fursa niliyopata na kwake wewe kwa kutazama kila wakati,” aliongeza.

Mnamo Jumatano, Julai 1, taarifa kutoka kampuni hiyo ilisema kuwa mlipuko wa coronavirus umeathiri pakubwa uchumi na hivyo basi italazimika kupunguza idadi ya wafanyikazi.

Ilisema hilo litatokana na kuwa watabadili mfumo wao wa kibishara ili kuzingatia ule wa kidijitali.

Haya yanajiri wiki chache baada kampuni ya Mediamax kuwafuta zaidi ya wafanyikazi 100 kazi.

Miongoni mwa waliopoteza kazi zao ni pamoja na mtangazaji Nancy Onyancha na mumewe Job Mwaura ambao wote walikuwa wakifanya kazi katika Televisheni ya K24.

Mbali na hao wawili, wafanyikazi wengine waliofutwa ni pamoja na Ken Wariahe (mtanagazaji nananga mhariri wa Kiswahili), Isabella Kituri (mtangazaji / mhariri wa Kiswahili), Caroline Wambui (mhariri mkuu wa Kiswahili), Shukri Wachu (mwandishi masuala ya elimu / uhalifu), Apollo Kamau (mwandishi wa masuala ya kisiasa ), Mercy Milanoi (mwandishi masuala ya biashara), Joy Kiruki (mhariri wa makala maalum), Gloria Milimu (mwandishi masuala ya afya) na Kimani Githuku (ripota).

Comments

comments

Trending