Kenya Kwanza waita Kalonzo ajiunge nao
NA SHABAN MAKOKHA
WANDANI wa Naibu Rais William Ruto wamemwalika kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kujiunga na muungano wao wa Kenya Kwanza ili kufanikisha azma yao ya kuunda serikali ijayo.
Walimshauri makamu huyo wa rais wa zamani kuweka kando mipango yake ya kufanya kazi na kiongo – zi wa ODM Raila Odinga wakimtaja kama kiongozi mwongo.
Seneta wa Bungoma Mo – ses Wetang’ula jana aliwaongoza wabunge kutoka vyama vya Amani National Congress (ANC), Ford Kenya na United Democratic Alliance (UDA) kuuza sera za muungano huo katika Kaunti ya Kakamega ambapo waliwataka wakazi kukatalia mbali muungano wa Azimio la Umoja.
Waliendesha kampeni katika maeneo bunge ya Navakholo na Ikolomani wakati ambapo Dkt Ruto angali anaendelea na ziara ya kujipigia debe nchini Amerika.
Seneta wa Kakamega Cleophas Malala alimhakikishia Bw Musyoka kwamba atapata mazingira yenye uaminifu ndani ya Kenya Kwanza chini ya uongozi wa Dkt Ruto, Bw Wetang’ula na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi.
“Umewahi kufanya kazi na Bw Odinga na badala yake ukadhulumiwa. Kwa mara nyingine umeonyesha nia ya kufanyakazi naye lakini anaonyesha ishara kwamba hataki kufanya kazi nawe. Je, lazima ufanye kazi naye ilhali kuna viongozi wengine ambao unaweza kufanya kazi nao?” akauliza Bw Malala.
Seneta huyo mbishi alisema ni makosa kwa Bw Musyoka kuachwa nje ya serikali ambayo itabuniwa na Dkt Ruto kwa ushirikiano na Mabw Mudavadi na Wetang’ula ambao waliteseka nao nchini ya uongozi wa Bw Odinga.
Bw Malala aliwashutu – mu magavana wanne kutoka eneo la magharibi, Wycliffe Oparanya (Kakamega), Wilbur Otichillo (Vihiga), Wycliffe Wangamati (Bungo – ma) na Sospeter Ojaamong (Busia) kwa kukataa kushirikiana na vyama vya ANC na Ford-Kenya.
“Ni makosa zaidi kwa magavana wetu kukuba – li kununuliwa na watu wengine kutoka nje ili kuhujumu mipango ya kisiasa ya kuwezesha jamii ya Mulembe kuingia serikali kupitia muungano wa Kenya Kwanza,” akaeleza.
Bw Wetang’ula alimta – ja Bw Odinga kama mwanasiasa mwongo na ambaye ameishiwa na mawazo mapya, huku akimshauri kustaafu kutoka siasa ili kupisha vizazi vya sasa.
Aliwaomba wakazi wa Kakamega na Wakenya kwa ujumla kumkataa kiongozi huyo wa ODM debeni mnamo Agosti 9, 2022.
“Ameishiwa kimawazo na hana kipya cha kuwasaidia Wakenya. Kumchagua kuwa Rais itakuwa sawa na kufungua ukurasa mpya katika taifa hili kwa kumpa Rais Uhuru Kenyatta nafasi ya kuongoza kwa muhula wa tatu kupitia mlango wa nyuma,” akasema Bw Wetang’ula ambaye pia ndiye kiongozi wa Ford Kenya.
Next article
Mauaji ya watu 11 yazua hofu Isiolo