Connect with us

General News

Kenya yafunzwa softball na Afrika Kusini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kenya yafunzwa softball na Afrika Kusini – Taifa Leo

Kenya yafunzwa softball na Afrika Kusini

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya Kenya ya mchezo wa softball iligundua bado ina safari ndefu ya kuwa mshindani baada ya kupoteza michuano mitano bila jibu dhidi ya Afrika Kusini kwenye kampeni za kuingia Kombe la Dunia U23.

Kwenye mashindano hayo ya Afrika, Kenya iliaibishwa katika mechi ya ufunguzi 10-0 mnamo Februari 8 na 20-2, 15-0, 24-0 na 22-2 Februari 9 mjini Pretoria.

Afrika Kusini ilinyakua tiketi hiyo moja kushiriki Kombe la Dunia U23 litakalofanyika Oktoba 22-30 mjini Parana, Argentina.

Wenyeji wa kombe hilo la Afrika pia walitawazwa mabingwa wa kwanza kabisa wa Afrika wa mchezo wa softball wa kitengo kipya cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23.

Kombe la Afrika la watu wazima lilianza Februari 10 likikutanisha Afrika Kusini, Kenya na Botswana. Washindi watajikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia mjini Auckland, New Zealand litakaloandaliwa Novemba 26 hadi Desemba 4 mwaka huu.