[ad_1]
Kenya yarejelea uuzaji mifugo Oman
Na ANTHONY KITIMO
KENYA imerejesha usafirishaji wa mifugo hadi nchi za kigeni baada ya kupigwa marufuku kwa miaka 16. Kutokana na hatua hiyo, kundi la kwanza la zaidi ya mifugo 40,000 wenye thamani ya Sh200 milioni liliondoka kwenye Bandari ya Mombasa jana alasiri kuelekea Oman, Mashariki ya Kati.
Hii ni baada ya nchi hizo mbili kukubali kushirikiana ili kuimarisha sekta ya ufugaji. Balozi wa Kenya, Mohammed Dor, alisema Oman ina uwezo wa kupokea zaidi ya mifugo 500,000 kutokana na ukubwa wa soko. “Leo tumeanzisha rasmi usafirishaji wa mifugo Oman.
Hii ni biashara nzuri na itainua uchumi wa nchi,” akasema balozi huyo. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mifugo ya kusafirishwa, balozi huyo alisema hatua hiyo inafuata sheria zilizowekwa na serikali ya Kenya ya kuhakikisha mbuzi, kondoo au ng’ombe wanaosafirishwa hawana magonjwa.
“Ajenda kuu ya nchi hizi mbili ni kuimarisha sekta ya ufugaji na kuinua uchumi. Hii ndiyo maana serikali za nchi hizo mbili zikaamua kushirikiana.”
Next article
TAHARIRI: Benki ziboreshe mitambo yake kuokoa wateja
[ad_2]
Source link