Connect with us

General News

Kenya yatahadhari polio ikigunduliwa Malawi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kenya yatahadhari polio ikigunduliwa Malawi – Taifa Leo

Kenya yatahadhari polio ikigunduliwa Malawi

NA AMINA WAKO

SERIKALI ya Kenya imechukua tahadhari baada ya maradhi ya polio kugunduliwa katika jiji kuu la Lilongwe, Malawi.

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), kisa hicho ndicho cha kwanza cha polio kugunduliwa Afrika katika muda wa zaidi ya miaka mitano.

Dkt Peter Borus, anayesimamia maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu (Kemri) ambaye pia anafanya kazi na WHO, alisema kuwa uchunguzi umeimarishwa katika vituo vyote vya kuingia nchini.

Aidha, Dkt Borus alisema kuwa wataalamu wa polio watakutana kesho kujadili na kuchunguza hali ya maandalizi nchini kuhusu jinsi ya kukabiliana na kisa chochote cha polio kikizuka.

“Tayari tumepokea ilani ya polio na tumetayarisha kila kitu kinachohusiana na uangalizi.

Kundi linaloshughulikia polio nchini vilevile litakutana kesho kuhakikisha kila kitu kiko shwari iwapo virusi hivyo vitagunduliwa nchini,” alisema Dr Borus.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending