Connect with us

General News

KHU yahitaji Sh20m kuandaa vipusa kwa hoki ya Jumuiya ya Madola – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

KHU yahitaji Sh20m kuandaa vipusa kwa hoki ya Jumuiya ya Madola

KHU yahitaji Sh20m kuandaa vipusa kwa hoki ya Jumuiya ya Madola

Na AGNES MAKHANDIA

Shirikisho la Mpira wa Magongo Kenya (KHU) lina bajeti ya Sh20 milioni kuandaa timu ya taifa ya wanawake kwa michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Birmingham, Uingereza mnamo Julai 29 hadi Agosti 8. 

Ikitangaza mabadiliko kwenye benchi ya kiufundi ya timu hiyo, KHU ilisema kuwa mamilioni hayo ya fedha yataisaidia kujiandaa kisawasawa kwa mashindano hayo ambayo Kenya itakutana na Australia, New Zealand, Scotland na Afrika Kusini katika Kundi B.

 “Tukipata usaidizi huo wa kifedha kwa muda unaofaa, tutajipima nguvu dhidi ya Ghana na Bangladesh ili tupate kujua utayari wetu,” aliongeza mwenyekiti wa shirikisho hilo, Nashon Randiek jijini Nairobi.

Alisema kuwa kwa sasa kikosi kinajumuisha wachezaji 46. “Tuna miezi mitatu ya kujitayarisha. Tunatumai kuchagua kikosi imara cha wachezaji 18 watakaotuwakilisha Uingereza,” alisema. Jacqueline Mwangi anasalia kocha mkuu na kusaidiwa na Barbra Simiyu naye Glennis Namasake ni meneja wa timu.

Maafisa wapya ni makocha Michael Malungu kutoka klabu ya Western Jaguars na Joseph Osino kutoka Butali Sugar Warriors atakayekuwa kocha wa makipa.

Mwanaolimpiki Manjit Singh ndiye mkurugenzi nao Rebecca Mueni na Vincent Muriki ni wanyooshaji wa misuli. Randiek na naibu mwenyekiti Elynah Shiveka watakuwa afisa mkuu wa kiufundi na mlezi mtawalia.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE