Connect with us

General News

Kigame arai Wakenya kuchagua Rais mcha Mungu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kigame arai Wakenya kuchagua Rais mcha Mungu – Taifa Leo

Kigame arai Wakenya kuchagua Rais mcha Mungu

NA CHARLES WASONGA

MGOMBEAJI wa urais Reuben Kigame amewataka Wakenya kuchagua rais mwadilifu na mcha Mungu ambaye atayapa kipaumbele maslahi ya wananchi.

Akiongea Jumatatu usiku kwenye mahojiano katika mojawapo ya televisheni nchini, Bw Kigame, ambaye ni msanii wa nyimbo za injili, alisema Kenya inahitaji viongozi wanaofanya maamuzi kutoka mioyo yao wala sio akilini mwao pekee.

“Labda wakati umetimu kwa nchi hii kuwa na uongozi unaotoka moyoni. Uongozi unaoweka Mungu na watu mbele kabla ya faida zozote zile kama vile miundo msingi. Kiongozi ambaye atalisha watu 2.8 milioni wanaokeketwa na njaa badala ya kujenga barabara ya expressway,” akasema.

Aliongeza kuwa si vibaya kwa kiongozi kujenga miundomsingi bali aangalie ikiwa juhudi zake zinasaidia au kuongezea raia mizigo.