– Ngunjiri alisema Kimunya hakuwepo wakati walikuwa wakileta mageuzi ndani ya chama cha Jubilee
– Orodha za watakaoshikilia nyadhifa kwenye kamati mbali mbali yalikataliwa kwenye bunge
– Tofauti zinaonekana kuibuka kati ya wandani wa Rais Uhuru na upande wa ODM kuhusu wanakamati bungeni
Kiongozi mpya wa wengi bungeni Amos Kimunya ameanza kazi yake kwa changamoto baada ya mapendekezo yake kuhusuwanachama wa kamati mbali mbali kukataliwa.
Inaarifiwa Kimunya alikuwa akiongoza mkutano kuhusu kuundwa kwa mojawapo wa kamati za bunge wakati tofauti zilizuka.
Kiongozi mpya wa wengi bungeni Amos Kimunya. KImunya alianza kibarua chake cha kwanza bungeni. Picha: Standard Source: UGC
Pande za Kieleweke na ule wa ODM zilizua masuala kuhusu baadhi ya wanachama wa kamati hiyo wakisema ni wandani wa Naibu Rais William Ruto.
Hata hivyo, Kimunya alishikilia kuwa ilikuwa ni haki ya kila mbunge kuhudumu kwenye kamati akiongeza kuwa Rais Uhuru Kenyatta ana habari kuhusu orodha hiyo.
“Tulifikiria kuwa Kimunya amebadilika na kuwa mnyenyekevu, lakini mkutano huo ulidhibitisha bado ni yule yule,” mbunge mmoja alisema.
Mbunge Ngunjiri Wambugu amemkosoa kiongozi mpya wa wengi Amos Kimunya. Alisema Kimunya haelewi kazi aliyopewa. Picha: Nation Source: UGC
“Alikataa kutuskiza na kulazimisha kuhusu orodha hiyo mpaka alipoiwasilisha kwenye bunge na kukataliwa,” aliongeza mbunge huyo.
Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu alisema tatizo la Kimunya ni kuwa alipewa wadhiwa ambao haukumfaa.
“Kiongozi mpya wa wengi bungeni Mheshimiwa Amos Kimunya hana habari kuhusu tulipotoka na kufikia sasa. Alipewa basi ambalo limejazwa mafuta na liko barabara iliyotiwa lami,” alisema Wambugu.