Connect with us

General News

Kinara wa zamani wa NSSF na wakuu wa kampuni ya hisa kupigwa faini ya Sh12.6 bilioni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kinara wa zamani wa NSSF na wakuu wa kampuni ya hisa kupigwa faini ya Sh12.6 bilioni – Taifa Leo

Kinara wa zamani wa NSSF na wakuu wa kampuni ya hisa kupigwa faini ya Sh12.6 bilioni

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA meneja wa uwekezaji katika Hazina ya Kitaifa Malipo ya Uzeeni (NSSF) na wafanyakazi watatu wa kampuni ya kununua na kuuza hisa iliyofilisika wamepatikana na hatia ya ulaghai wa Sh1.4million.

Kiongozi wa mashtaka aliomba mahahakama ya kuamua kesi za ufisadi iwatoze faini ya Sh4.2bilioni kila mmoja na pamoja na kusukuma jela kifungo kisichopungua miaka 10.

Hakimu mkuu Bw Lawrence Mugambi aliwapata na hatia Francis Zuriels Moturi (aliyekuwa meneja wa uwekezaki NSSF), David Ndirangu (NSSF) na maafisa wa kampuni ya Discount Securities Ltd (DSL) Wilfred Mungoro (mkurugenzi wa masuala ya fedha) na Isaac Nyakundi,(aliyekuwa meneja wa uwekezaji DSL ya kula njama za kuiba kutoka kwA NSSF wakidai waliekeza katika hisa.

“Naomba hii mahakama iwatoze faini ya Sh4.2bilioni kila mmoja kwa kula njama za kuilaghai NSSF Sh1.4bilioni wakidai wataziwekeza katika biashara ya hisa,” kiongozi wa mashtaka alisihi hakimu mkuu Bw Lawrence Mugambi.

Vinara wa kampuni iliyofilisika ya DSL wakiwa kortini Januari 28, 2022. PICHA/ RICHARD MUNGUTI

Bi Hellen Mutela alimweleza Bw Mugambi kwamba chini ya sheria za hujuma za kiuchumi mshtakiwa utozwa faini mara tatu ya kiwango cha pesa alichoiba.

Lakini mawakili wanaowatetea washtakiwa hao waliomba wapewe muda wa kujitetea.

Bw Mugambi alikubaliana na wakili wa washtakiwa kwamba anahitaji muda wa kuandaa malilio kabla ya adhabu kupitishwa.

“Ili kuwapa muda washtakiwa waandae malilio yao kabla ya hukumu kupitishwa naamuru washtakiwa wazuiliwe katika kituo cha polisi cha Capitol hadi Jumatatu (Januari 31,2022),”Bw Mugambi aliamuru.

Akisoma uamuzi Bw Mugambi alisema upande wa mashtaka umethibitisha makosa dhidi ya washtakiwa kwa kuwasilisha ushahidi jinsi walifyoza NSSF kati ya 2004 na 2007 zaidi ya Sh1.6bilioni wakidai wataekeza kwa kununua hisa katika makampuni makuu saba nchini.

Moturi aliyestafu kutoka NSSF baada ya kuhitimu miaka 55 mnamo 2005 alipatikana na hatia katika mashtaka matatu.

Francis Moturi (kushoto) aliyepatikana na hatia ya ufujaji wa Sh1.4bn akiwa kizimbani na James Akoya na David Ndirangu walioachiliwa. PICHA/ RICHARD MUNGUTI 

Wakurugenzi wa DSL Ndirangu, Mungoro na Nyakundi walipatikana na hatia ya kula njama za kulaghai, undanganyifu, ufisadi na wizi.

Lakini mahakama iliwaachilia aliyekuwa meneja mkuu masuala ya fedha na uwekezaji James Akoya na aliyekuwa mkaguzi wa hesabu NSSF Bi Mary Ndirangu na kampuni ya Orchard Estates Ltd.

Bw Mugambi alisema washtakiwa hao wanne walikula njama njama za kuekeza kupitia kampuni ya  DSL iliyofilisika ikiwa na mabilioni ya pesa za umma.

Mashtaka mengine waliyopatikana na hatia ni kulipa pesa za wazee kwa njia ya ufisadi, kutofuata sheria za uwekezaji,kujinufaisha na mali ya umma kwa njia ya ufisadi,wizi na kutozingatia sheria katika usimamizi wa mali ya umma.

Wanne hao walikana walitekeleza uhalifu huo kati ya Agosti 2004 na Julai 20 2007 kwa kudai walinunua idadi kubwa ya hisa kwa niaba ya NSSF.

Mahakama ilifahamishwa NSSF iligeuzwa kuwa hazina ya malipo ya uzeeni 2003 kisha bodi ya wasimamizi wakaamua wawekeze pesa hizo za malipo ya uzeeni katika miradi ya kuiletea NSFF mapato.

Meneja wa NSSF walipendekeza wawekeze zaidi ya Sh1.6bilioni.

Lakini hatimaye wakuu wa NSSF waligudua kupitia uchunguzi wa shirika la uwekezaji (CDSC) pesa hizo (Sh1.6bilioni) hazikuwekezwa ila zilipotea.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending