Connect with us

General News

kinoti kufungwa miezi minne gerezani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

kinoti kufungwa miezi minne gerezani

kinoti kufungwa miezi minne gerezani

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) George Kinoti jana alisukumiwa kifungo cha miezi minne gerezani bila faini kwa kukaidi agizo la mahakama kuu amrudishie mfanyabiashara Jimmy Wanjigi bunduki saba zilizotwaliwa polisi walipovamia makazi yake mijini Nairobi na Mombasa.

Na wakati huo huo Jaji Antony Mrima alisema amekuwa akipokea vitisho endapo hatakoma kutoa maagizo makali dhidi ya maafisa wakuu serikalini “ataona cha mtema kuni.” Lakini Jaji Mrima alisema jana “hatakoma kutekeleza majukumu yake bila upendeleo au woga.”

Akiendelea kusikiza kesi hiyo dhidi ya Bw Kinoti, Jaji Mrima alisema alipokea vitisho na kuonywa ajihadhari anapotoa maamuzi dhidi ya maafisa wakuu serikalini. “Hivi majuzi nilisikiza kesi dhidi ya maafisa wakuu fulani serikalini na kutoa maagizo waadhibiwe lakini nilishangaa nilipopokea ujumbe kutoka kwa mmoja wao akinitisha na kunionya nijihadhari kutokana na msimamo waku,” alisema Jaji Mrima.

Jaji huyo aliendelea kusema , “Mjumbe aliyenifikishia ujume huo alinitisha nitajuta endapo sitakoma kutoa maagizo makali dhidi ya wakuu serikalini.”“Nilionywa vilkali nitaona cha mtema kuni endapo nitaendelea kushikilia msimamo wangu mkali,” alisema Jaji Mrima.

Akitoa uamuzi Jaji Mrima alimwamuru Bw Kinoti ajisalamishe mara moja katika idara ya magereza aanze kutumikia kifungo. Jaji huyo alisema ikiwa Bw Kinoti hatajisalamisha kwa idara ya magereza kutumikia kifungo Inspekta Jenerali Hilary Mutyambai atamsaka na kumtia nguvuni.

“Inspekta Jenerali wa polisi ameagizwa amtie nguvuni Kinoti na kumpeleka kutumikia kifungo,” aliagiza Jaji Mrima. Pia mahakama ilisema ikiwa kinara huyu wa DCI atakwepa siku ile atakapostaafu akamatwe na kupelekwa jela kutumikia kifungo hicho.

Mahakama ilitoa agizo baada ya kumpata Bw Kinoti na hatia ya kukaidi agizo la mahakama iliyotolewa Juni 21 2019. Mahakama ilikuwa imemwamuru DCI arudishe bunduki saba zilizotwaliwa na polisi waliovamia makazi ya mfanya biashara Bw Jimmy Wanjigi.

“In the further event the IG of Police fails to execute the warrant, the same shall remain valid and be executed anytime including when Kinoti leaves the office of the DCI,” said Judge Mrima. Jaji Mrima alitoa uamuzi huo katika kesi iliyoshtakiwa na Bw Wanjigi baada ya bunduki alizokuwa amepewa rasmi na Serikali zilizopotwaliwa.

Mahakama iliamuru arudishiwe silaha hizo lakini DCI alikataa kutekeleza agizo hilo. Mwezi uliopita Bw Kinot alikosa kufika kortini kisha ikaahirishwa hadi jana uamuzi uliposomwa kwa njia ya mtandao. Bw Wanjigi aliwakilishwa na wakili Willis Otieno ilhali Bw Kinoti aliwakilishwa na wakili wa Serikali.