Connect with us

General News

Kipa Steffen arefusha mkataba wake kambini mwa Man-City hadi 2025 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kipa Steffen arefusha mkataba wake kambini mwa Man-City hadi 2025 – Taifa Leo

Kipa Steffen arefusha mkataba wake kambini mwa Man-City hadi 2025

Na MASHIRIKA

KIPA Zack Steffen wa Manchester City ametia saini mkataba mpya wa miaka minne utakaomdumisha ugani Etihad hadi mwaka wa 2025.

Mlinda-lango huyo nambari moja katika timu ya taifa ya Amerika alijiunga na Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2019 na mkataba wake wa awali kambini mwa Man-City ulikuwa utamatike rasmi mnamo 2023.

Steffen, 26, amekuwa chaguo la pili baada ya Ederson Moraes uwanjani Etihad na amewajibishwa katika EPL mara mbili huku akisaidia waajiri wake kushinda taji la Carabao Cup mnamo 2020-21.

Steffen alijiunga na Man-City baada ya kuagana na Man-City kutoka Columbus Crew kabla ya kuhudumu kambini mwa Fortuna Dusseldorf katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) mnamo 2019-20.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO