Connect with us

General News

Kiswahili sasa kufundishwa nchini Ethiopia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kiswahili sasa kufundishwa nchini Ethiopia – Taifa Leo

Kiswahili sasa kufundishwa nchini Ethiopia

NA MASHIRIKA

KISWAHILI sasa kitaanza kufunzwa nchini Ethiopia siku chache baada ya lugha hiyo kuidhinishwa kutumika kuendesha shughuli rasmi za Umoja wa Afrika (AU).

Kiswahili kitaanza kufuzwa katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa ambacho kitashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salama cha Tanzania.

Profesa Tasew Woldehana wa Chuo Kikuu cha Addis Ababa jana alisema maandalizi ya kuanza kufundisha Kiswahili katika taasisi hiyo yamekamilika.

Taasisi hiyo imekumbatia Kiswahili huku hadhi ya lugha hiyo ikiendelea kupaa.

Baraza Kuu la Viongozi wa Afrika, wiki iliyopita, liliidhinisha Kiswahili kutumika kuendesha shughuli rasmi za AU. Hatua hiyo ilijiri baada ya Makamu wa Rais wa Tanzania Philip Mpango kuwasilisha ombi kwenye mkutano uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia, huku akisema kuwa mashirika ya kanda mbalimbali ya Afrika tayari yameidhinisha Kiswahili kuwa lugha rasmi.

Mpango alisema tayari Kiswahili kinatumiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Muungano wa Maendeleo wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Novemba, mwaka jana, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitangaza Julai 7 kuwa siku ya Kiswahili Duniani kila mwaka.

Tanzania wiki iliyopita, ilisihi China

kuanza kufunza Kiswahili katika taasisi zake.

Waziri wa Utamaduni Mohammed Mchengerwa aliwasilisha ombi hilo wiki iliyopita kwa balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian.

Waziri Mchengerwa alisema kuwa Tanzania iko tayari kutuma walimu kufundisha Kiswahili katika taifa hilo la Asia.

Alisema kuwa lugha ya Kichina tayari inafundishwa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma hivyo Wachina pia wanafaa kujifunza Kiswahili.

“Lugha ya Kiswahili inakua kwa kasi ndani na nje ya bara la Afrika.

Hivyo basi, ninasihi China kukumbatia lugha hiyo na kuifunza katika vyuo vyake,” akasema.

Serikali ya Tanzania pia imeagiza mabalozi kuanzisha madarasa ya kufundisha Kiswahili katika balozi zake zote kama njia mojawapo ya kukuza lugha hiyo na kupatia ajira walimu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki.

Inakadiriwa kuwa Kiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 kote duniani na tayari kinafunzwa katika nchi mbalimbali duniani. Kiswahili ni miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa na watu wengi zaidi duniani, kwa mujibu wa Unesco.

Afrika Kusini ndiyo nchi ya hivi karibuni ambayo imeruhusu kujumuishwa kwa Kiswahili katika mtaala wake wa elimu.

Mnamo Disemba 2019, serikali ya Uganda iliagiza Kiswahili kufundishwa katika shule zote za msingi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending