Connect with us

General News

Kiungo Nafula atoka Vihiga Queens kuyoyomea Urusi kujiunga na Kayserispor – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kiungo Nafula atoka Vihiga Queens kuyoyomea Urusi kujiunga na Kayserispor – Taifa Leo

Kiungo Nafula atoka Vihiga Queens kuyoyomea Urusi kujiunga na Kayserispor

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Christine Nafula amejiunga na klabu ya Kayserispor nchini Uturuki, Ijumaa.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 ametokea mabingwa wa zamani wa Kenya, Vihiga Queens.

Ametangaza makao hayo yake mapya kupitia mtandao wake wa kijamii akisema, “Timu mpya, changamoto mpya. Kazi ianze sasa.”

Nafula anawakilishwa na maajenti wa LTA ambao pia wana washambulizi Wakenya Jentrix Shikangwa na Tereza Engesha kama wateja wao.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Harambee Starlets alikuwa katika klabu ya AE Larissa kwenye Ligi Kuu ya Wanawake ya Ugiriki kabla ya kuingia Vihiga Queens na kushinda nao tuzo ya timu bora ya wanawake kwenye tuzo za SOYA mwezi Januari 2022.

Nafula, ambaye amewahi kuchezea Dalheim nchini Uswidi, alikuwa katika kikosi cha Starlets kilichoshiriki Kombe la Afrika (AWCON) kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2016 nchini Cameroon.

Yeye ni Mkenya wa nne kucheza Uturuki baada ya Esse Akida aliyekuwa Besiktas mwaka 2020, Mwanahalima Adam anasakatia Hakkarigucu naye Shikangwa alijiunga na Fatih Karagumruk mwezi Januari 2022 kwa kandarasi ya mwaka mmoja.

Fatih Karagumruk, Hakkarigucu na Kayserispor zinashikilia nafasi ya pili, nne na 11 kwenye Ligi Kuu ya Uturuki kundi B.