Connect with us

General News

Kiwanda cha betri kufungwa baada ya marufuku ya vyuma – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kiwanda cha betri kufungwa baada ya marufuku ya vyuma – Taifa Leo

Kiwanda cha betri kufungwa baada ya marufuku ya vyuma

NA DAVID MWERE

ATHARI za marufuku ambayo Rais Uhuru Kenyatta aliweka dhidi ya biashara ya vyuma vikuu kuu zimeanza kujitokeza kiwanda kimoja cha kutengeneza betri humu nchini kikikabiliwa na hatari ya kufungwa.

Kufungwa kwa kiwanda cha Associated Battery Manufacturers (ABM), kilichoko Athi River kutachangia maelfu ya wafanyakazi wake kupoteza ajira, ambao wao hukitegemea kukimu mahitaji ya familia zao.

Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo Bw Guy Jack alionya kuwa kitengo chake cha kuyeyusha vyuma na betri kuu kuu ili kutengeneza bidhaa nyinginezo pia kitafungwa kwa kukosa malighafi.

“ABM, yenye maelfu ya wafanyakazi walioajiriwa moja kwa moja inaelekea kufungwa kutokana na ukosefu wa raslimali,” Bw Jack akasema.

“Hatutaendelea na shughuli za kawaida endapo agizo la Rais la kupiga marufuku biashara ya vyuma vikuukuu haifafanuliwa na utawala wa eneo hili,” akawaambia wanahabari Ijumaa.

Afisa huyo alisema kwamba kampuni hiyo inaka – biliwa na uhaba wa malighafi kwa sababu maafisa wa usalama, na wale serikali ya kaunti, walifasiri visivyo marufuku hiyo ya Rais Kenyatta.

Bw Jack anahofia kwamba marufuku hiyo itaathiri pakubwa wafanyabiashara wa humu nchini na viwanda vinavyotegemea vyuma vikuuvikuu kutengeneza bidhaa mbalimbali.