Connect with us

General News

Kizaazaa Old Trafford Man Utd ikivizia Spurs – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kizaazaa Old Trafford Man Utd ikivizia Spurs – Taifa Leo

Kizaazaa Old Trafford Man Utd ikivizia Spurs

NA MASHIRIKA

LONDON, UINGEREZA

MANCHESTER United na Liverpool zinatarajiwa kuwa miba kwa Tottenham Hotspur na Brighton mtawalia kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, leo Jumamosi.

United wako namba tano kwa alama 47 kutokana na mechi 28 – wamejibwaga uwanjani mara mbili zaidi ya Spurs, iliyo alama mbili nyuma katika nafasi ya saba.

Red Devils wameambulia alama moja kutoka mechi mbili zilizopita dhidi ya Watford na viongozi Manchester City.

Nao Spurs wamejaa motisha baada ya kulipua Leeds na Everton kwa jumla ya magoli 9-0.

United ya kocha Ralf Rangnick imechapa Spurs mara mbili mfululizo, lakini jijini London.

United ilipigwa nyumbani kama nyoka 6-1 na Spurs zilipokutana Old Trafford mara ya mwisho mnamo Oktoba 2020; kupitia mabao ya Harry Kane na Son Heung-min (mawili kila mmoja) na Tanguy Ndombele na Serge Aurier.

Macho yatakuwa kwa Kane na Son huku Cristiano Ronaldo na Jadon Sancho wakitegemewa na United.

Masaibu ya nambari 13 Brighton yanatarajiwa kuongezeka dhidi ya nambari mbili Liverpool inayofukuza City.

Brighton imepoteza makali yaliyoduwaza Liverpool 1-0 mnamo Februari 2021 na pia kuwalazimisha 2-2 Oktoba ugani Anfield.

Timu ya Brighton pia ilitoka 1-1 dhidi ya vijana wa kocha Jurgen Klopp mara ya mwisho ugani Amex mnamo Novemba 2020.

Wavamizi matata Mohamed Salah na Sadio Mane wataongoza mashambulizi ya Liverpool.

Neal Maupay na Danny Welbeck watategemewa na Brighton.

Katika michuano iliyosakatwa Alhamisi usiku, Chelsea ililipua wenyeji Norwich 3-1.

Nao Newcastle walizoa ushindi wa tatu mfululizo kwa kupepeta wenyeji Southampton 2-1.

Kambini mwa Aston Villa, Philippe Coutinho aliendelea kung’ara baada ya kufungua ukurasa wa magoli wakibwaga wenyeji Leeds 3-0.

Leeds wananing’inia pabaya kufuatia vichapo sita mfululizo.

Kwa upande wao, Wolves walimaliza mikosi ya kupoteza mechi tatu mfululizo kwa kung’ata Watford 4-0 ugani Molineux. Leo pia itakuwa zamu ya Brentford kualika Burnley jijini London.