Connect with us

General News

Korti yaruhusu kuapishwa Kananu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Korti yaruhusu kuapishwa Kananu – Taifa Leo

Korti yaruhusu kuapishwa Kananu

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA ya Juu jana ilifutilia mbali agizo la kuzuia kuapishwa kwa Bi Anne Kananu kuwa Gavana wa Nairobi.

Sasa Bi Kananu ataapishwa wakati wowote baada ya kufutiliwa mbali kwa agizo la kuzima kuapishwa kwake. Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko aliwasilisha ombi katika mahakama hii ya upeo akidai uteuzi wa Bi Kananu kutwaa wadhifa wa ugavana Nairobi hakukufanywa kwa mujibu wa sheria.

Katika uamuzi wao Majaji Mohamed Ibrahim,Smokin Wanjala,Njoki Ndung’u ,Isaac Lenaola na William Ouko walisema ombi la Bw Sonko la kupinga kuapishwa kwa Bi Kananu halina mashiko kisheria. Majaji hao walisema wametilia maanani ushahidi aliowasilisha Bw Sonko kupinga kuapishwa kwa Bi Kananu kuchukua wadhifa wa Gavana Nairobi na kufikia uamuzi hauna uzito wowote kisheria.

Wakili Duncan Okatchi aliyewakilisha Bi Kananu aliomba mahakama hiyo ifutilie mbali kesi ya Bw Sonko aliyoshtaki Oktoba 25, 2021 akisema “rufaa aliyowasilisha katika mahakama ya rufaa hiajaamuliwa. Itasikizwa Novemba 22,2021.”

Bw Okatchi alisema hakuna suala kutoka mahakamaya rufaa ambayo inaweza kuamuliwa na Mahakama ya Juu. Majaji hao walisema hakuna kesi yoyote iliyowasilishwa na Bw Sonko inayostahili kuamuliwa na Mahakama ya Juu.

Majaji hao watano walisema kulingana kifungu nambari 163 (4)(a) cha Katiba wanaweza tu kuamua suala tu linalopasa kutafsiriwa. Katika kesi ya Bw Sonko, Majaji hao watano walisema kesi ya gavana haijaimbua suala ambalo linaweza kutafsiriwa na mahakama hii ya upeo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending