Connect with us

General News

KPA yaponea kupoteza ardhi bandarini Lamu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

KPA yaponea kupoteza ardhi bandarini Lamu – Taifa Leo

KPA yaponea kupoteza ardhi bandarini Lamu

NA BRIAN OCHARO

MAMLAKA ya Bandari za Kenya (KPA) imepata afueni baada ya mahakama kusitisha kwa muda agizo lililozuia shirika hilo kutumia sehemu ya ardhi ndani ya mradi wa bandari ya Lamu.

Majaji Stephen Kairu, Pauline Nyamweya na Jessie Lesiit wa Mahakama ya Rufaa walisema agizo la kuzuia KPA kutumia sehemu hiyo ya ardhi inayozozaniwa na kampuni ya kibinafsi, litakiuka maslahi ya umma kwa vile mabilioni ya pesa za umma zishatumiwa katika mradi huo.

Mzozo ulikuwa umeibuka wakati Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC) ilipokosa kulipa fidia kwa kampuni ya Nightshade Properties Ltd, ambayo ardhi yake ya ekari 100 iliyo Mokowe, Kaunti ya Lamu, ilikuwa imetwaliwa kwa lazima katika ujenzi wa bandari.

Majaji pia walisema KPA imethibitisha kuwa, ujenzi uliofanywa katika sehemu hiyo ya ardhi ni kubwa mno, umetumia muda mwingi na kiasi kikubwa cha pesa.

Walikubaliana na shirika hilo kwamba kutakuwa na hasara zisizoweza kurekebishwa baadaye ikiwa mahakama ya rufaa isingetoa agizo la kubatilisha uamuzi uliokuwa umetolewa na mahama ya mazingira na ardhi ambapo KPA ingefurushwa kutoka katika sehemu hiyo.

“Uamuzi wetu ni kuwa tumeridhishwa na ombi la KPA kutaka agizo la awali libatilishwe hadi rufaa isikilizwe na kuamuliwa.

Kwa msingi huo, utekelezaji wa agizo lililotolewa na mahakama ya mazingira na ardhi mnamo Machi 23, 2021, umesitishwa,” wakasema majaji.

Ujenzi mbalimbali unaosaidia shughuli za bandari ya Lamu umetekelezwa katika kipande hicho cha ardhi ikiwamo sehemu za meli kutia nanga na afisi za wasimamizi wa bandari.

Ujenzi Kwa mujibu wa KPA, ujenzi huo uligharimu serikali takriban Sh992.4 milioni kwa hivyo haitakuwa haki kwao kufurushwa kwa sababu ya mzozo wa fidia.

Mwaka uliopita, NLC iliagizwa na mahakama ya mazingira na ardhi kuitisha mkutano kabla ya siku 45 kukamilika ili kukubaliana kiasi cha fidia ambacho kampuni husika ilistahili kulipwa.

Agizo hilo lililotolewa na Jaji James Olola katika Mahakama ya Malindi, lilitaka NLC, Mamlaka ya Kustawisha miradi ya Lapsset na KPA ziondoke katika sehemu hiyo ya ardhi wakishindwa muafaka kuhusu fidia katika wakati uliotolewa kwao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending