Connect with us

General News

Kulala chini ya saa 5 kwa siku kutakugeuza bwege chumbani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kulala chini ya saa 5 kwa siku kutakugeuza bwege chumbani – Taifa Leo

MUME KIGONGO: Kulala chini ya saa 5 kwa siku kutakugeuza bwege chumbani

NA LEONARD ONYANGO

KUKOSA msukumo wa kufanya mapenzi miongoni mwa wanaume kumekuwa kukihusishwa na baadhi ya vyakula, kutofanya mazoezi, ubugiaji wa pombe, mihadarati na matatizo ya kiafya kama vile kisukari, msongo wa mawazo, upungufu wa damu mwilini (anemia) na unene kupindukia.

Lakini sasa wataalamu wanasema kuwa kutolala usingizi wa kutosha kunasababisha wanaume kukosa hamu ya mapenzi.

Tafiti mbalimbali za hivi karibuni zinaonyesha kuwa kulala chini ya masaa matano kwa siku kunasababisha homoni za testosterone kupungua.

Homoni hizo ndizo hufanya wanaume kuwa na msukumo wa kutaka kufanya mapenzi na kuwezesha mwili kuzalisha mbegu za kiume. Aidha husaidia vijana wa kiume kuwa na misuli na mifupa imara.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Chicago nchini Amerika, ulibaini kuwa wanaume ambao wamekuwa wakilala chini ya masaa matano, walikuwa na kiwango kidogo cha homoni hizo ikilinganishwa na wenzao waliolala muda mrefu.

Kulingana na watafiti hao, vijana wa kiume wasiolala usingizi wa kutosha pia wako katika hatari ya kuwa na misuli na mifupa hafifu, kukasirika kiholela na udhaifu wa mwili kwa jumla.

Hata hivyo, tatizo la upungufu wa testosterone, linaweza kutibiwa hospitalini na kupitia kubadilisha mtindo wa maisha kwa kula vyakula vifaavyo, kuepuka pombe na kufanya mazoezi ya viungo.

Baadhi ya vyakula vinavyoongeza homoni hizo ni samaki, mboga kama vile spinachi, parachichi (avokado), mayai, nafaka, asali, kabichi, maziwa kati ya vinginevyo.

Kabichi ina kemikali inayojulikana kama indole-3-carbinol ambayo husaidia homoni hizo kufanya kazi vyema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending