Connect with us

General News

Kumbe UDA ni mali binafsi ya mwanzilishi kama ODM! – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kumbe UDA ni mali binafsi ya mwanzilishi kama ODM! – Taifa Leo

WANDERI KAMAU: Kumbe UDA ni mali binafsi ya mwanzilishi kama ODM!

NA WANDERI KAMAU

KWA yeyote ambaye hufuatilia kwa ukaribu mwelekeo wa siasa za Amerika, Uingereza, Ujerumani, Canada na mataifa mengine yaliyostawi kidemokrasia, ni vigumu kueleza viongozi wa vyama vikuu tawala.

Nchini Amerika, kwa mfano, umaarufu wa vyama kama Republican na Democratic mtawalia hujitokeza pakubwa kuliko viongozi tofauti wanaovitumia kuwania urais.

Nchini Uingereza, umaarufu wa vyama vya Labour ama Congress hufunika sifa za wanasiasa wanaovitumia kuwania uongozi, kama vile Uwaziri Mkuu.

Isitoshe, wanasiasa hao hufuata kanuni na taratibu zinazowekwa na taasisi mbalimbali za vyama hivyo kuhusu vile wanavyopaswa kuendesha kampeni zao.

Hata hivyo, hali ni kinyume Kenya na bara Afrika kwa jumla. Vyama vya kisiasa huwa kama mali ya vigogo wa kisiasa waliovianzisha. Alipoanzisha chama cha UDA mwishoni mwa 2020, Naibu Rais William Ruto aliahidi kwamba “kitakuwa chama cha kila Mkenya, bila kujali asili, tabaka, jamii au dini yake.”

Alikitaja kuwa chama cha “mahasla”; yaani watu wa kawaida, ambao wanategemea kazi zao za kila siku kupata riziki yao.

Alikita chama hicho kwenye msingi huo ili kukitofautisha na vyama vingine vya kisiasa nchini, ambavyo vimekuwa vikiongozwa na kudhibitiwa na watu matajiri pekee bila kushirikisha walalahoi. Kinyume na ahadi za Dkt Ruto, imeibuka kuwa Kenya ina safari ndefu kuzifikia nchi kama Amerika, kutenganisha vyama na waanzilishi wake.

Hilo lilidhihirishwa na mamia ya wawaniaji waliojitokeza kulalamikia taratibu zilizotumika kuendesha shughuli za mchujo wa chama hicho Alhamisi wiki iliyopita.

Baadhi walilalamikia majina ya wanachama kukosekana kwenye Sajili Kuu ya Chama, wengine wakadai baadhi ya wagombeaji walikuwa wakiwahonga wanachama huku baadhi ya wanasiasa wakilaumiwa kuuteka mchakato mzima wa mchujo.

Licha ya hakikisho na ahadi za Dkt Ruto, imedhihirika wazi kuwa, vyama vya kisiasa nchini vitabaki ‘mali’ ya majukwaa ya wanasiasa kujijenga wenyewe.

Kabla ya UDA kuandaa mchujo huo, Dkt Ruto na washirika wake walikuwa wakitoa kila aina ya lawama, hasa dhidi ya kiongozi wa ODM, Raila Odinga, wakimtaja kuwa “mmiliki, mwendeshaji na mwamuzi wa masuala yote yanayohusu ODM.”

Je, Dkt Ruto anawezaje kujitakasa kutokana na matatizo yaliyoandama mchujo wa UDA? Hawezi hata kidogo!

Wito mkuu kwa Wakenya ni kuziiga Amerika au Uingereza—kwa kukuza vyama huru visivyodhibitiwa na wanasiasa kwa namna yoyote ile.

[email protected]

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending