Connect with us

General News

Kuria abadili nia, sasa atawania ugavana Kiambu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kuria abadili nia, sasa atawania ugavana Kiambu – Taifa Leo

Kuria abadili nia, sasa atawania ugavana Kiambu

Na CECIL ODONGO

MBUNGE wa Gatundu Kusini, Bw Moses Kuria ameghairi nia yake ya kutowania cheo chochote kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 baada ya kujitosa kwenye kiny’ang’anyiro cha ugavana wa Kaunti ya Kiambu.

Bw Kuria kupitia akaunti zake za mitando ya kijamii hapo Jumamosi, alisema amesukumwa na wito wa wafuasi wake kuwa awanie kiti hicho na akamwomba mwenyezi Mungu amwongoze kupata ushindi.

“Sauti ya watu ndiyo sauti ya Mungu. Nisaidie mwenyezi Mungu kwa kuwa chini ya mbawa zako nahisi kusitiriwa na kuwa salama,” akaandika Bw Kuria kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Agosti 31, 2021, mbunge huyo aliye ni kinara wa Chama Cha Kazi (CCK) alitangaza kuwa hangewania cheo chochote katika uchaguzi ujao kwa kuwa lengo lake ni kujenga na kuvumisha chama chake na pia kupigania maslahi ya wakazi wa Mlima Kenya.

“Nimeamua kuwa sitawania cheo chochote cha kisiasa 2022. Ninamakinikia kujenga Chama Cha Kazi ambacho kinazingatia sana maslahi ya watu wa Mlima Kenya,” akasema Bw Kuria wakati huo.

Amehudumu kama mbunge kwa mihula miwili kupitia TNA na Jubilee.

Mchuano wa kusaka ugavana Kiambu sasa utashuhudia ushindani mkali ikizingatiwa, Gavana wa sasa James Nyoro analenga kuhifadhi kiti chake.

Wengine ni gavana wa kwanza William Kabogo na gavana aliyebanduliwa Ferdinand Waititu.