Connect with us

General News

Kwa kupigia chapuo ‘six-piece’ Raila amejitokeza kama kiongozi asiyezingatia ahadi kwa wenzake – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kwa kupigia chapuo ‘six-piece’ Raila amejitokeza kama kiongozi asiyezingatia ahadi kwa wenzake – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Kwa kupigia chapuo ‘six-piece’ Raila amejitokeza kama kiongozi asiyezingatia ahadi kwa wenzake

MNAMO Aprili 18, 2022 mwaniaji urais wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga alitoa wito wa wakazi wa ngome yake ya Luo Nyanza kuwachagua wawaniaji viti kwa tiketi ya ODM pekee katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Akiongea katika hafla ya mazishi ya aliyekuwa Balozi wa Kenya nchini Qatar marehemu Paddy Ahenda katika eneobunge la Kabondo Kasipul, kaunti ya Homa Bay, Bw Odinga aliwahimiza wakazi kuwachagua wawaniaji wa ODM katika viti vyote sita; kuanzia urais hadi udiwani.

Bw Odinga aliwataja wale wanaowania kwa vyama vingine (vikiwemo vile vilivyoko ndani ya Azimio) kama “maadui” ambao wanapania kugawanya eneo hilo kuelekea uchaguzi huo.

Lakini Bw Odinga asije akasahau kwamba, Aprili 7, 2022 alitangaza kufutuliwa mbali kwa mfumo huo wa uchaguzi, maarufu kama ‘six-piece’.

Bw Odinga alisema vyama vyote tanzu katika Azimio vitakuwa huru kudhamini wagombeaji maeneo yote nchini.

Kwa kuenda kinyume na ahadi hiyo, mnamo Jumapili wiki jana, Bw Odinga amejitokeza kama kiongozi asiyezingatia ahadi kwa wenzake.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending