Connect with us

General News

Laini za simu ambazo bado hazijasajiliwa kuzimwa Aprili – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Laini za simu ambazo bado hazijasajiliwa kuzimwa Aprili – Taifa Leo

Laini za simu ambazo bado hazijasajiliwa kuzimwa Aprili

NA KENYA NEWS AGENCY

LAINI za simu ambazo hazijasajiliwa zitazimwa mwezi ujao, Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA) imeonya.

Mamlaka hiyo imewataka Wakenya ambao laini zao hazijasajiliwa kuzisajili kabla ya makataa ya mwishoni mwa Aprili 2022.

Bw Julius Lenaseiyan, afisa wa utekelezaji wa sheria za CA, anasema kuwa kumekuwa na ongezeko la watu wanaotumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa nchini.

Kanuni hizo mpya za CA zinalenga kupunguza visa ambapo laini za simu zinatumiwa katika uhalifu na kisha kutupwa.

Kwa mujibu wa CA, laini nyingi zilizoanza kutumiwa kabla ya 2015 hazijasajiliwa kwa sababu hakukuwa na sheria kuhusiana na usajili wa laini wakati huo.

“Kanuni za 2015 sasa zinalazimu kampuni za kutoa huduma za simu kama vile Safaricom, Airtel, Telkom kusajili laini na kunasa picha za wateja,” akasema Bw Lenaseiyan.

Sheria inahitaji mtu anayetaka kusajili laini kutoa kitambulisho au paspoti kwa raia wa kigeni.

“Mawakala wa kampuni za kutoa huduma za simu, wanatakiwa kuwa makini kuhakikisha kuwa stakabadhi zinazotolewa ni halali,” akasema.

Mamlaka hiyo imetoa makataa hayo huku visa vya ulaghai kwa kutumia simu vikiwa vimeongezeka kwa kasi nchini.

Wahalifu hao huzima laini hizo baada ya kuzitumia kulaghai waathiriwa.

Baadhi ya wahalifu pia hutumia vitambulisho vilivyopotea kusajili laini za simu na kisha kuzitumia katika shughuli za uhalifu.

Mamlaka hiyo ilisema kuwa itaanza kukagua mitambo ya kuhifadhi taarifa za usajili wa wateja ya kampuni za simu katika juhudi za kutaka kuhakikisha kuwa sheria inazingatiwa.

“Kampuni za simu pia zitahitaji kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kwa CA kuhusu namna zinavyotekeleza sheria ya usajili,” akasema Bw Lenaseiyan.

Alionya kuwa mawakala wanaokiuka sheria ya usajili wa wateja wanaonunua laini watakamatwa na kushtakiwa.

Mapema mwezi huu Machi, CA ilisema kuwa inapanga kuzima laini ambazo hazijasajiliwa Aprili 15, 2022.

CA imekuwa ikitishia kufunga laini ambazo hazijasajiliwa tangu 2012.

Lakini jana ilijitetea kuwa mpango wake wa kufunga laini ambazo hazijasajiliwa umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara baada ya kampuni za simu kuomba muda zaidi.

“Mamlaka sasa inatoa makataa na tunasihi kampuni za mawasiliano ya simu kuhakikisha kuwa wateja wao wanasajiliwa kabla ya laini zao kufungwa,” akasema Bw Lenaseiyan.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending