Mkurugenzi Mkuu wa Maabara ya Lancet Ahmed Kalebi ametangaza kuchukua likizo kutoka katika mitandao ya kijamii ili aishugulikie maabara yake ambayo imeshtumiwa kwa kutoa matokeo tatanishi
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe aliagiza maabara hiyo ifanyiwe uchunguzi na kuonya maabara mengine kuwa yatafungwa endapo yatatoa matokeo yenye utata ya virusi vya COVID-19.
Mkurugenzi Mkuu wa Maabara ya Lancet Ahmed Kalebi Source: UGC
” Ni ukweli maabara ya Lancet ilitoa matokeo tatanishi, maabara hiyo ilithibitisha kuwa wagonjwa walikuwa na virusi vya COVID-19 lakini baada ya kupimwa tena katika maabara ya KEMRI ilibainika kuwa wagonjwa hawakuwa na virusi hivyo,” Alisema Kagwe.
Taarifa ya Kagwe inajiri baada ya wafanyakazi 18 wa shule ya kifahari St. Andrews Turi kupatikana na virusi vya Covid-19 baada ya kufanyiwa vipimo katika maabara ya Lancet.
Baada ya matokeo hayo kufanyiwa tena ukaguzi katika maabara ya KEMRI, ilibainika kuwa wafanyakazi hao hawakuwa na virusi vya COVID-19.
Waziri Kagwe aliagiza maabara hiyo ifanyiwe uchunguzi na kuonya maabara mengine kuwa yatafungwa endapo yatatoa matokeo yenye utata ya virusi vya COVID-19. Source: Facebook
Inaonekana ufichuzi wa waziri Kagwe umemkwaza Mkurugezi Mkuu wa maabara hiyo Bw. Kalebi ambaye amesema hatakuwa mitandoni kwa muda usiojulikana.
” Kwa mashabiki wangu wote, ningependa kuwataarifu kuwa najipa likizo kutoka mitandaoni kwa muda wa siku kadhaa ili niweze kuishughulikia maabara yangu kwa ajili ya kupigana vita dhidi ya janga hili la corona, tungependa kutoa matokeo ya ukweli na kuepukana na kisanga kilichotupata awali,” Alisema Kalebi.
Aidha, Waziri Kagwe ametishia kufunga maabara ya Lancet iwapo itapatikana na hatia.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.