Connect with us

General News

Leicester wakomoa Liverpool na kuwaweka Man-City katika nafasi nzuri ya kuhifadhi ubingwa wa EPL – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Leicester wakomoa Liverpool na kuwaweka Man-City katika nafasi nzuri ya kuhifadhi ubingwa wa EPL – Taifa Leo

Leicester wakomoa Liverpool na kuwaweka Man-City katika nafasi nzuri ya kuhifadhi ubingwa wa EPL

Na MASHIRIKA

MKUFUNZI Jurgen Klopp amesema Liverpool sasa watakuwa na presha tele ya kufikia Manchester City kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kikosi chake kupokezwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Leicester City mnamo Jumanne usiku ugani King Power.

Goli la Leicester katika mchuano huo lilifumwa wavuni na Ademola Lookman katika dakika ya 59, muda mfupi baada ya kutokea benchi.

Liverpool kwa sasa wanajivunia alama 41 wanakabiliwa na presha ya kuhimili ushindani mkali kutoka kwa Chelsea na Man-City ambao ni mabingwa watetezi wa EPL. Chelsea wanakamata nafasi ya tatu kwa alama 41 huku Man-City wakiselelea kileleni mwa alama 47. Hata hivyo, wawili hao watamenyana na Brighton na Brentford mtawalia usiku wa Disemba 29, 2021.

“Sikufurahishwa kabisa na matokeo yetu dhidi ya Leicester. Hatuko sawa kwenye msimamo wa jedwali na kichapo tulichopokezwa sasa kitawapa Man-City motisha ya kufungua mwanya mkubwa zaidi wa alama kileleni,” akasema Klopp aliyeashiria kutamauka kwenye vita vya kuwania ufalme wa EPL muhula huu.

Mechi hiyo hiyo ilikuwa ya kwanza kati ya 29 zilizopita ligini kwa Liverpool kukamilisha bila kufunga bao. Aidha, ulikuwa mchuano wa pili kati ya 19 ya hadi kufikia sasa kwenye kampeni za EPL msimu huu kwa Liverpool kupoteza baada ya kushinda 12 na kuambulia sare mara tano.

Liverpool waliopoteza nafasi nafasi nyingi za wazi, ikiwemo penalti ya Mohamed Salah iliyopanguliwa na kipa Kasper Schmeichel, sasa watakuwa na ulazima wa kutandika Chelsea mnamo Jumapili ugani Stamford Bridge ili kuweka hai matumaini ya kutwaa taji la EPL muhula huu. Salah sasa anakamilisha kampeni za mwaka huu wa 2021 akijivunia mabao 24 na kuchangia mengine 11 katika EPL.

Leicester waliokosa idadi kubwa ya wanasoka wa kikosi cha kwanza kutokana na majeraha na ugonjwa wa Covid-19, walishuka dimbani wakiwa na kiu ya kulipiza kisasi dhidi ya Liverpool waliowadengua kwenye robo-fainali za Carabao Cup wiki moja iliyopita.

Mabingwa hao watetezi wa Kombe la FA sasa wanakamata nafasi ya tisa kwa alama 25 sawa na Wolves. Mechi dhidi ya Liverpool ilikuwa yao ya pili kushinda kati ya saba zilizopita.

Hadi waliposhuka ulingoni kuvaana na Leicester, Liverpool walikuwa wakijivunia rekodi ya kufunga mabao 50 kutokana na mechi 18 za EPL. Leicester walikuwa wamepachika wavuni magoli 12 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa tena mara 12 kutokana na mechi nne za awali. Mbili kati ya mechi hizo ni kwenye sare ya 3-3 dhidi ya Liverpool katika Carabao Cup ugani Anfield na kichapo cha 6-3 kutoka kwa Man-City ligini mnamo Jumapili iliyopita ugani Etihad.

MATOKEO YA EPL (Jumanne):

Palace 3-0 Norwich

Southampton 1-1 Tottenham

Watford 1-4 West Ham

Leicester 1-0 Liverpool

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending