Connect with us

General News

Linturi akamatwa kwa kutoa matamshi ya uchochezi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Linturi akamatwa kwa kutoa matamshi ya uchochezi – Taifa Leo

Linturi akamatwa kwa kutoa matamshi ya uchochezi

Na CHARLES WASONGA

SENETA wa Meru Mithika Linturi amekamatwa Jumapili asubuhi kutokana na matamshi ya chuki aliyotoa mkutano wa kisiasa mjini Eldoret Jumamosi.

Hii ni kufuatia agizo la Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kwa Inspekta Jenerali Hillary Mutyambai kumchunguza Bw Linturi kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi katika mkutano ulioongozwa na Naibu Rais Dkt William Ruto.

Akiongea mjini Eldoret Bw Linturi anadaiwa kusema hivi: “Enyi watu wa Uasin Gishu, msicheze na Kenya. Kile nawaomba ni kwamba mhakikishe kuwa mumeondoa madoadoa hapa kwenu.”

Kauli hiyo ilifasiriwa kuashiria kuwa alikuwa akiwachochea wenyeji dhidi ya wale wakazi ambao sio wa asili ya kaunti hiyo, kwa sababu za kisiasa.

Hii ndio maana Bw Haji akaamuru polisi ichunguze matamshi hayo kubaini ikiwa yalilenga kuchochea uhasama wa kisiasa au la. Hii ni ikizingatiwa kuwa eneo hilo lilishuhudia mapigano ya kisiasa baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.

Hata hivyo, Bw Linturi amejitetea akisema kuwa alilenga kuwashauri wakazi wasiwachague wanasiasa ambao wamemuasi Naibu Rais William Ruto na kuamua kuunga mkono wanasiasa wengine.

Mwanasiasa huyo anadaiwa kutoa matamshi hayo katika Eldoret Sports Club katika mkutano ambapo Wazee na wakazi wa Uasin Gishu walimpa baraka Dkt Ruto anapowania urais mwaka huu.

Seneta huyo anatarajiwa kufikishwa Nairobi leo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending