Connect with us

General News

Lowassa alazwa tena hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Lowassa alazwa tena hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji – Taifa Leo

Lowassa alazwa tena hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji

Na CITIZEN

DAR ES SALAAM, TANZANIA

ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Tanzania na mgombeaji urais katika uchaguzi mkuu wa 2015, Edward Lowassa amelazwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Muhimbili kwa matibabu baada ya kuugua.

Kulingana na duru za familia yake, Bw Lowassa alifanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo siku tano zilizopita lakini akapata matatizo ikabidi arejeshwe.

“Alifanyiwa upasuaji tumboni lakini kwa bahati mbaya akapata matatizo zaidi. Lakini sasa yuko katika hali nzuri na anaendelea kupata nafuu,” mwanawe wa kiume, Fred Lowassa, akasema Ijumaa jioni bila kutoa maelezo zaidi.

Bw Lowassa, 68, alihudumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania kati ya mwaka wa 2005 hadi 2008, chini ya utawala wa Rais wa zamani Jakaya Kikwete, kabla ya kulazimishwa kujiuzulu.

Kabla ya hapo, Lowassa alishikilia wadhifa wa Waziri katika Afisi ya Waziri Mkuu katika muhula wa pili wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Alishindania tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili awe mgombeaji wake wa urais, lakini aliondolewa mapema na Rais wa zamani Julius Nyerere, aliyamini kuwa Lowassa “hakuwa amehitimu kuwa Rais.”

Alidumisha kiti chake cha ubunge na kuhudumu kama mbunge hadi 1997 alipoteuliwa kuwa Waziri katika Afisi ya Makamu wa Rais anayesimamia Mazingira na Vita dhidi ya Umasikini.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 2000, Lowassa aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Mifugo na kuacha kumbukumbu kama waziri mchapa kazi.

Mnamo 2005 mwanasiasa huyo aliamua kutosaka tiketi ya urais kupitia chama cha CCM lakini baadaye akaamua kuwa kiongozi wa kampeni za urais za Jakaya Kikwete.

Mnamo 2014 Lowassa alipigwa marufuku kushiriki shughuli za CCM kwa muda wa mwaka mmoja, kwa kosa la kuanza kampeni za urais mapema kabla ya muda ulioruhusiwa.

Mnamo Mei 2015, Bw Lowassa hatimaye alizindua kampeni yake ya urais mjini Arusha, lakini akafeli kupata tiketi ya CCM.

Ni baada ya hapo ambapo alijiunga na chama cha Upinzani Chadema na kupata tiketi ya kuwania urais.

Hata hiyo alishindwa na mgombeaji wa CCM John Pombe Magufuli.