[ad_1]
Maafisa 30 kujiuzulu Nandi kugombea viti vya kisiasa 2022
Na TOM MATOKE
WAFANYAKAZI wakuu zaidi ya 30 katika serikali ya kaunti ta Nandi wanapanga kujiuzulu Februari 2022 kugombea viti tofauti kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.
Hatua hii itavuruga serikali ya Gavana Stephen Sang ambaye atakuwa akitetea kiti chake.
Maafisa wa umma wanaomezea mate viti kwenye uchaguzi mkuu wako na hadi Februari kujiuzulu ikiwa ni miezi sita kabla ya tarehe ya uchaguzi.
Tayari, waziri wa biashara katika serikali ya kaunti ya Nandi Jacob Tanui ametangaza kuwa atagombea kiti cha ubunge cha Mosop kwa tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA).
Mkurugenzi wa kaunti hiyo wa Kilimo Dkt Daniel Rono ananuia kugombea kiti cha ubunge cha Kesses kaunti ta Uasin Gishu County huku Daniel Kogo, afisa katika ofisi ya gavana akimezea mate kiti cha useneta kaunti ya Nandi.
Karani wa usimamizi wa kaunti ya Nandi Philistia Maiyo anagombea kiti cha eneobunge la Aldai kinachoshikiliwa na Cornelius Serem.
Wengine wanaotamani viti tofauti ni Peter lelei na Isaac Maritim (ubunge, Tinderet), John Suge kutoka wizara ya Afya (wadi ya Chemeili/Chemase).
Mkurugenzi wa Utamaduni Cosmas Kipchumba anagombea kiti cha udiwani wadi ya Lelmokwo Ngecheck.
Gavana Sanga tayari amewataka maafisa wa serikali yake wanaotaka kugombea viti kwenye uchaguzi mkuu kujiuzulu ili aweze kupanga upya serikali yake kwa kipindi kitakachosalia.
[ad_2]
Source link