Connect with us

General News

Maafisa wa IEBC katika maeneobunge na kaunti wahamishwa kuepusha wizi wa kura – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Maafisa wa IEBC katika maeneobunge na kaunti wahamishwa kuepusha wizi wa kura – Taifa Leo

Maafisa wa IEBC katika maeneobunge na kaunti wahamishwa kuepusha wizi wa kura

SIAGO CECE NA KNA

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), inahamisha wafanyakazi wake wote wanaohudumu katika afisi za kaunti na maeneobunge ili kuzuia visa vyovyote vya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Naibu Mwenyekiti wa IEBC, Bi Juliana Cherera, alisema tume hiyo inataka kuziba mianya yote ambayo huenda ikaibua malalamishi kutoka kwa wanasiasa kuhusu kutofanikishwa kwa uchaguzi huru na wa haki.

“Wale waliohudumu katika Uchaguzi Mkuu wa 2017 katika kaunti au eneobunge wanaweza kushawishiwa vibaya kwa urahisi, ndiposa tunawapeleka wakahudumie vituo vingine tofauti katika uchaguzi wa Agosti 9,” akasema, alipokuwa katika eneo la Diani, Kaunti ya Kwale.

Hata hivyo, Bi Cherera alieleza kuwa IEBC huwa na sera inayohitaji wafanyakazi wake kuhamishwa miezi michache kabla uchaguzi uandaliwe kwa hivyo si jambo jipya.

“Hii ni kuhakikisha kuna uwajibikaji na uwazi katika shughuli nzima ya uchaguzi,” akasema.

Alisisitiza kuwa, tume hiyo inayosimamiwa na Bw Wafula Chebukati, inajitahidi kuhakikisha kutakuwa na rasilimali zote za kutosha uchaguzini ili kuepusha changamoto zinazoweza kufanya shughuli hiyo ikose kuaminika.

Bi Cherera alikuwa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa ‘Uchaguzi Bila Balaa’ unaosimamiwa na shirika la Human Rights Agenda (HURIA).

Mpango huo unahusisha hamasisho la kuepusha ghasia za kisiasa.

Wakati huo huo, IEBC ilisema imepunguza ada za uteuzi kwa wanawake na makundi mengine maalumu kama vile walemavu.

Kulingana na Bi Cherera, tume inaelewa changamoto ambazo wanawake wanaowania nafasi tofauti wanapitia hivyo basi imenuia kuwapunguzia mzigo.

Naibu Mwenyekiti huyo alisema wanaume wanaowania viti vya urais, watalipa Sh200,000 huku wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu wakilipa Sh100,000.

Wagombeaji ugavana na useneta ambao ni wanaume watalipa Sh50,000, na wanawake Sh25,000. Pia aliwakumbusha wanasiasa ambao hawajafaulu katika kura za uteuzi wa vyama kuwa wana muda hadi Mei 2, kuwasilisha karatasi zao kama wagombeaji huru.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending