Maafisa wa trafiki wameagizwa kutoweka vizuizi katika barabara kuu za jijini.
Taarifa kutoka afisi ya Naibu Inspekta Generali Edward Mbugua ilisema sababu kuu ya agizo hilo ni kwa kuwa barabara nyingi zinatumika katika kuendeleza ufisadi.
Maafisa wa trafiki wakisimamisha gari. Source: UGC
“Sio jambo geni kuwa vizuizi hivyo vinatumika katika kuwafaidi maafisa na makamanda wao ambao wanashiriki ufisadi,”Mbugua alisema kulingana na ripoti ya Daily Nation.
Badala yake, Mbugua alisema maafisa hao wanapaswa kuzunguka katika barabara kuu wakishika doria na wala sio kupiga kambi mahali pamoja.