Connect with us

General News

Maafisa walaumiwa kwa kuzembea – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Maafisa walaumiwa kwa kuzembea – Taifa Leo

Bidhaa: Maafisa walaumiwa kwa kuzembea

Na SIAGO CECE

MAAFISA WA USALAMA katika mpaka wa Kenya na Tanzania wamekashifiwa kwa kuzembea na kusababisha uingizaji wa bidhaa ghushi nchini.

Bidhaa hizo ambazo zinajumuisha sukari, mchele, sabuni ya unga na makoroni, huingizwa nchini kupitia mipaka ya Vanga, Lungalunga na Shimoni katika Kaunti ya Kwale.Wafanyabiashara walaghai husafirisha bidhaa hizo kwa kutumia boti, pikipiki na njia nyingine za vichochoroni.

Katika eneo la Shimoni, kuna zaidi ya sehemu tano ambazo wao hutumia ilhali sehemu moja pekee ndiyo huwa na maafisa wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA).Sehemu hizo ni Kinuyuni, Mazaro, Bati, Kiwambale na Mwambale ambazo zote ziko katika ufuo wa Bahari Hindi.

Imebainika kuwa, wakati mwingi bidhaa hizo huingizwa usiku wa manane na ifikapo saa kumi na moja alfajiri polisi wanapowasili, huwa zishapelekwa kwingine.Wiki iliyopita, Mshirikishi wa Eneo la Pwani, Bw John Elungata, aliagiza msako uanzishwe dhidi ya uingizaji wa bidhaa haramu nchini.

“Tunataka kuwe na mbinu kali zaidi ili bidhaa zote haramu zinaswe katika maeneo ya mipaka ili tudhihirishe kuwa tuko chonjo,” akasema alipokutana na maafisa wa usalama. Lungalunga.Kulingana naye, uingizaji wa bidhaa haramu nchini huathiri sana uchumi wa nchi hasa kwa wafanyabiashara halali.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending