Connect with us

General News

Maandalizi ya KCPE, KCSE yakamilika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Maandalizi ya KCPE, KCSE yakamilika – Taifa Leo

Maandalizi ya KCPE, KCSE yakamilika

FAITH NYAMAI NA MWANGI MUIRURI

WAZIRI wa Elimu Profesa George Magoha jana alitangaza kuwa maandalizi ya mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE yamekamilika huku KCSE ikitarajiwa kuanza wiki ijayo.

Akitangaza hayo, Profesa Magoha aliwaonya wanafunzi dhidi ya kushiriki migomo kuelekea mitihani hiyo na badala yake akawataka wamakinikie masomo yao kwa sababu udanganyifu hautavumiliwa kamwe .

Hapo jana, Profesa Magoha alisisitiza kuwa mitihani yote imehifadhiwa salama wakati alipowakabidhi wakurugenzi wa elimu kwenye kaunti mbalimbali funguo za makontena ambayo mitihani hiyo imehifadhiwa.

“Hadi sasa, hakuna mtihani ambao umeibwa. Wale ambao wanalenga kununua karatasi ya mitihani eti ni mtihani halisi, wasifanye hivyo kwa sababu yote imehifadhiwa salama,” akasema Profesa Magoha akizungumza katika Chuo cha Serikali cha KSG.

KCSE inatarajiwa kuanza mnamo Februari 28 na kukamilika Aprili 1 huku KCPE ikifanyika kutoka Machi 7 hadi Machi 9.

“Kwa wanafunzi ambao wanapanga kuchoma mali ya shule kabla ya mitihani hiyo kuanza, tutafunga shule hizo kisha wafanye mitihani chini ya mti,” akasema Profesa Magoha.

Afisa Mkuu Mtendaji wa KNEC David Njengere naye alitangaza kuwa mwaka huu watahiniwa 1,225, 507 watafanya mtihani wa KCPE katika vituo 28, 316 kote nchini ikilinganishwa na 1, 191, 752 waliofanya mtihani katika vituo 28, 467 mnamo 2020.

Wanafunzi 831,015 nao wamejisajili katika vituo 10,413 kufanya mtihani wa KCSE. Hii ni ongezeko la watahiniwa 78,034 ambao ni sawa na asilimia 9.39.

Wakati huo huo, Profe – sa Magoha ameonya ku – wa kuna njama ya baadhi

ya wanakandarasi na wasimamizi wa miradi ya kujenga madarasa kuilaghai serikali Sh4.12 bilioni.

Pesa hizo zinalenga kutumika katika kukamilisha ujenzi wa madarasa ya kutumika katika kutekeleza na mafunzo ya Mtaala wa Umilisi na Utendaji (CBC). Profesa Magoha, alisema wizara ya elimu imeweka Sh788,000 kama gharama ya kuweka paa la darasa moja ilhali baadhi ya wanakandarasi wanataka walipwe Sh412,000 zaidi.

Alikariri kuwa serikali bado inalenga kutekeleza ahadi yake ya kuyajenga madarasa 10,000 kutumika na wanafunzi kwa masomo ya CBC kufikia Juni mwaka huu.

“Nataka niweke wazi kuwa hatutavumilia utapeli huu. Kwa wanakandarasi wanaoshiriki njama hiyo, wafahamu kuwa tutalipa tu pesa tulizotenga kwa mradi huo wala hatutaongeza hata senti,” akasema Profesa Magoha.

Alikuwa akizungumza alipozuru maeneobunge ya Maragua na Gatanga. Pia alisisitiza kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa 6,500 lazima ikamilike kufikia mnamo Machi mwaka huu.