[ad_1]
Macho kwa Obiri akiendea mamilioni ya fedha Ras Al Khaimah Half Marathon
Na GEOFFREY ANENE
Bingwa wa Great North Run Hellen Obiri atakuwa kwenye mizani ya Waethiopia atakapotimka Ras Al Khaimah Half Marathon nchini Milki za Kiarabu, Jumamosi.
Mshikilizi huyo wa rekodi za kitaifa za maili moja, mita 3,000 na mita 5,000 analenga kuimarisha muda wake bora katika nusu-marathon kutoka saa 1:04:51 ambao unaweza kutosha kumpa taji la Ras Al Khaimah. Mwanadada wa mwisho kutoka Kenya kushinda ni Fancy Chemutai mwaka 2018.
Mbali na Obiri, kuna Sheila Chepkirui, Daisy Cherotich, Judith Jeptum, Pauline Esikon, Abel Kipchumba, Alexander Mutiso, Philemon Kiplimo, Daniel Kibet, Kennedy Kimutai, Kelvin Kiptum, Mathew Kimeli na Rodgers Kwemoi, miongoni mwa wengine. Bingwa wa 2013 Geoffrey Kamworor na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya marathon Brigid Kosgei walijiondoa siku chache zilizopita.
Mashindano hayo yanarejea baada ya kuahirishwa kutoka 2021 kwa sababu ya mkurupuko wa virusi vya corona. Washindi wa kitengo cha wanaume na pia wanawake watatia mfukoni Sh1.5 milioni kila mmoja. Mkenya Kibiwott Kandie na Muethiopia Ababel Yeshaneh waliibuka washindi 2020.
Next article
Prisons Mombasa inajipatia miaka mitatu kushiriki kipute…
[ad_2]
Source link