Connect with us

General News

Macho yetu yako kwa Uhuru, IEBC na Knec 2022 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Macho yetu yako kwa Uhuru, IEBC na Knec 2022 – Taifa Leo

TAHARIRI: Macho yetu yako kwa Uhuru, IEBC na Knec 2022

Na MHARIRI

MWAKA huu wa 2022 utakuwa wa shughuli tele. Macho ya Wakenya yataelekezwa hasa kwa Rais Uhuru Kenyatta, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na Baraza la Mitihani la Kitaifa (Knec).

Rais Kenyatta anatarajiwa kuongeza juhudi kuhakikisha kwamba miradi yake aliyoanzisha tangu alipochukua hatamu za uongozi 2013, inakamilika kabla ya kustaafu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.

Huku zikiwa zimesalia siku 218 kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao, Rais Kenyatta angali na muda wa kutosha kuweka misingi kabambe ya kufufua uchumi uliolemazwa na janga la virusi vya corona.

Kiongozi wa nchi pia hana budi kuhakikisha kwamba ujenzi wa madarasa mapya 10,000 yatakayotumiwa na wanafunzi wa Sekondari ya Awali (Junior Secondary) chini ya Mtaala wa Umilisi na Utendaji (CBC), yanakamilika kabla ya Agosti.

Madarasa hayo yasipokamilishwa mapema, wanafunzi watakaojiunga na Sekondari ya Awali mwaka ujao huenda wakalazimika kusomea chini ya miti.

Rais Kenyatta pia anakabiliwa na kibarua kigumu kuhakikisha kuwa Wakenya hawagawanywi na mawimbi ya kisiasa yanayoendelea nchini.

Maafisa wa usalama ambao watahusika pakubwa kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao utakuwa wa amani hawana budi kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao bila kuegemea mrengo wowote wa kisiasa.

Tume ya IEBC inatarajiwa kugonga vichwa vya habari mara kwa mara mwaka huu huku ikiendelea kujiandaa kuhakikisha kwamba uchaguzi ujao unakuwa huru na haki.

IEBC ni sharti idhihirishie Wakenya kwamba imejiandaa vyema kusimamia Uchaguzi Mkuu ujao.

Mizozo kuhusu kandarasi ya vifaa vya kupigia kura ishughulikiwe kwa haraka ili isije ikatatiza maandalizi ya uchaguzi Mkuu ujao.

Aidha, IEBC inafaa kutumia mamlaka iliyopewa na sheria kuadhibu wanasiasa wanaojihusisha na michango ya harambee na kampeni za mapema.

Baraza la Knec, kwa mara ya kwanza, litaandaa mitihani ya kitaifa mara tatu ndani ya mwaka mmoja.

Baraza hilo tayari limetangaza kuwa litaandaa mitihani ya Darasa la Nane (KCPE) na Kidato cha Nne (KCSE) Machi na Desemba, 2022.

Vilevile, baraza hilo litaandaa mtihani wa Gredi 6 kwa wanafunzi wa CBC. Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) na Knec zihakikishe kuwa watahiniwa wanaandaliwa vyema.Kwako msomaji wetu, tunakutakia Mwaka Mpya wenye heri na fanaka.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending