– Rais wa nchi hiyo Andry Rajoelina alikuwa amedai kuwa amepata dawa ya kutibu ugonjwa wa corona
– Kwa sasa nchi hiyo imeweka amri ya kutotoka nje baada ya visa vingi vya maambukizi ya ugonjwa huo kuripotiwa
– Jumamosi Julai 4, nchi hiyo ilirekodi visa 216 vya maambukizi ya virusi hivyo baada ya watu 675 kufanyiwa vipimo
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameuwekea mji mkuu wa Antananarivo masharti mapya ya kutotoka nje kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya COVID-19, miezi miwili tu baada ya masharti hayo kuondolewa.
Madagascar imekuwa ikirekodi visa vichache vya ugonjwa wa corona ila kwa sasa idadi hiyo imeongezeka kwa kasi.
Jumamosi Julai 4, nchi hiyo ilirekodi visa 216 vya maambukizi ya virusi hivyo baada ya watu 675 kufanyiwa vipimo.