Wahudumu wanane walijiuzulu wiki jana kutokana na kushinikizwa na familia zao ambazo zilikuwa na wasiwasi kuwa watapeleka virusi hivyo nyumbani na kuwaambukiza jamaa zao.
Kulingana na Profesa Mayen Machut Achiek ambaye anasimamia jopo kazi la COVID-19, alisema siku ya Jumapili, Julai 13, kuwa wanane hao ni ikiwemo wanne wa usafi na wauguzi wanne.
Baadhi yao wanadaiwa kusita kuripoti kazini baada ya kuogopeshwa na namna wagonjwa wa COVID-19 walivyokuwa wakiangamia.
Profesa Mayen Machut Achiek ambaye anasimamia jopo kazi la COVID-19 Sudan Kusini. Picha:CitizenDaily. Source: Facebook
“Wakati huu ambapo watu wengi wanapoteza maisha yao kutokana na Covid-19, wahudumu wa afya wamekimbia,”
“Wamejiuzulu kwa sababu ya shinikizo ya familia. Lakini endapo watarejea basi itabidi tumewatumia kwa sababu tunahitaji kila mtu. Hospitali zote za Sudan Kusini zimeathirika na haya, ukienda katika hospitali za wilaya, utawapata madaktari wakiwa na wasiwasi,” Achiek aliwaambia waandishi wa habari jijini Juba.
Profesa Mayen Machut Achiek pia aliahiid kuwa serikali ya Sudan Kusini itatoa vifaa vya kujilinda kwa wahudumu wa afya. Source: Getty Images
Machut Achiek pia aliongezea kuwa wizara ya afya itatoa vifaa vya kujilinda kutoka kwa wadhamini kwa wahudumu wa afya ambao wako kwenye mstari wa mbele kukabili ugonjwa huo.
Kufikia sasa, Sudan Kusini imethibitisha visa 2,139 huku Kenya ikiwa na visa 10, 294 kwa jumla.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu wengine 12 wamefariki dunia kutokana na virusi vya COVID-19.
Kagwe alisema Kenya kwa sasa imerekodi vifo 197 kwa jumla na visa 189 vipya vya maambukizi vimeripotiwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.