Connect with us

General News

Madume wa KU wataka kushiriki dimba la Afrika Mashariki katika Handiboli – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Madume wa KU wataka kushiriki dimba la Afrika Mashariki katika Handiboli – Taifa Leo

Madume wa KU wataka kushiriki dimba la Afrika Mashariki katika Handiboli

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya wanaume ya Chuo cha Kenyatta (KU) ya mchezo wa handiboli inasadikiza kuwa imekaa vizuri kujikaza mithili ya mchwa ili kuhifadhi taji la kitaifa baina ya vyuo vikuu nchini (KUSA) muhula huu.

KU ni kati ya vikosi ambavyo hutoa upinzani mkali kwenye mechi za Ligi Kuu nchini (KHF). KU chini ya nahodha, Samuel Katuva inajivunia kutawazwa mabingwa katika ngarambe ya KUSA msimu uliyopita. Pia ni miongoni mwa vikosi ambavyo vimekuza wachezaji wengi tu na kusajiliwa na klabu za ligi kuu nchini.

”Mwaka jana niliteuliwa naibu wa kocha kisha mwaka huu ndio nimeteuliwa kushiriki wadhifa wa kocha mkuu lakini kwa jinsi nimetazama wachezaji wangu wana uwezo wa kufanya vizuri kwenye mashindano tofauti nchini,” alisema kocha wake, Victor Luvale ambaye ni mchezaji wa Black Mamba. Kocha huyo husaidiana nao Catherine Cherotich na Robert Osano.

Super Cup

KU wakati iliwahi jivunia kufanya vizuri kwenye mechi za ligi kuu ilikuwa msimu wa 2013/14 ambapo iliibuka ya pili na kufuzu kushiriki kinyang’anyiro cha Super Cup. Kwenye mechi za KUSA anasema kuwa anafahamu wapinzani wao wamejipanga kuwakabili kwa udi na uvumba. ”Kiukweli tunaamini tumepanga wachezaji wetu vizuri na tayari kuteremsha ushindani wa kufa mtu.”

Fainali za KUSA

Katika michuano ya KUSA kanda ya Nairobi msimu uliyokamilika mwezi umepitia, KU ilimaliza kileleni na kufuzu kushiriki fainali za kitaifa zilizopigiwa kwenye chuo kikuu cha Eldoret. Katika fainali KU ilizaba Jomo Kenyatta (JKUAT) mabao 26-19. Katika nusu fainali, KU ilivuna mabao 26-23 dhidi ya Mt Kenya (MKU) nayo JKUAT ilinyuka Chuo cha Eldoret (UoE).

Wachezaji wa timu ya KU wakijadiliana kabla ya kuingia dimbani kushiriki mechi ya ligi kuu…
Picha/JOHN KIMWERE

Kwenye utangulizi wa mechi za ligi ya KUSA Kanda ya Nairobi muhula huu leo Jumamosi, wasomi wa KU wamepangwa kufungua kampeni zake dhidi ya GRESTA. Kocha Catherine Cherotich anasema anatamani sana kuona KU chini ya uongozi wao ikimaliza kati ya nne bora kwenye kampeni za ligi kuu ndani ya miaka mitano ijayo.

”Pia ninataka tufuzu kushiriki mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati hivi karibuni,” kocha huyo alisema na kuongeza kuwa itakuwa furaha kwake akiongoza kikosi hicho kushiriki kipute hicho. KU inajivunia kuchangia mchezaji mmoja Titus Kipruto kuteuliwa katika timu ya taifa mwaka 2019.

Idadi ya wachezaji waliowahi kchezea KU walipokuwa wanafunzi chuoni humo na kujiunga na timu zingine inajumuisha:Dennis Magoiya, Victor Luvale, Charles Malema, Titus Kipruto, Dennis Munjera na Patrick Njagi wote Black Mamba.

Clinton Maiko, Nicholas Okore, William Malui, Snox Collins na Brian Wakukha wote Halmashauri ya Nafaka na Mazao nchini (NCPB). Pia wapo Shel Kuya na Bethuel Kiptoo wa Kahawa na Buccaneers mtawalia.

KU inajumuisha:Samuel Katuva (nahodha), Morgan Simiyu (naibu wa nahodha), Julius Chiunda, Dickson Wanyama, Fresnel Khisa, Donald Idaho, Onesmus Aron, Amos Keter na Isaac Nyongesa. Pia wapo Phelix Ongoro, Harrison Mwadali, Willis Musembi, Isaiah Wafula na Wenceslaus Ochieng.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending