Connect with us

General News

Maeneo 8 ya kuamua rais mpya katika 2022 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Maeneo 8 ya kuamua rais mpya katika 2022

Maeneo 8 ya kuamua rais mpya katika 2022

Na LEONARD ONYANGO

NAIBU RAIS William Ruto, kinara wa ODM Raila Odinga na wawaniaji wengine wa urais, watahitajika kuimarisha kampeni zao katika maeneo hayo ili kuhakikisha wanajipatia sehemu kubwa ya kura milioni kura milioni 8.9.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), jumla ya wapigakura wapya 1,519,294 walisajiliwa, na kufikisha jumla ya wapigakura milioni 21.1.Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alisema daftari la wapigakura linatarajiwa kukaguliwa ili kuondoa majina ya wafu kabla ya kuchapisha kwenye Gazeti Rasmi la Serikali majina ya wapigakura halisi watakaoshiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Nairobi iliongoza kwa kusajili wapigakura wapya 152,920 na kufanya idadi ya watu waliojisajili kufikia milioni 2.4. Kaunti za Nakuru na Kiambu zilifuatia kwa kusajili wapigakura wapya 62,064 na 59,813 mtawalia katika shughuli ya usajili wa wapigakura kwa wingi iliyokamilika Ijumaa iliyopita. Uchambuzi wa kina wa wapigakura unaonyesha kuwa, iwapo Naibu Rais atafanikiwa kupata zaidi ya asilimia 90 ya kura katika maeneo ya Bonde la Ufa na Mlima Kenya, huenda akamlemea mpinzani wake mkuu Bw Odinga.

Eneo la Bonde la Ufa, ikiwemo Kaunti ya Nakuru pamoja na eneo la Mlima Kenya likijumuisha Kaunti ya Laikipia, yana jumla ya kura milioni 8.9.Eneo la Bonde la Ufa – zikiwemo Kaunti za Kajiado, Narok na Samburu – lina jumla ya kura milioni 4.3. Japo baadhi ya wanasiasa kutoka eneo la Mlima Kenya; Spika wa Bunge Justin Muturi na Gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria wametangaza kuwania urais, wadadisi wanasema sehemu kubwa ya kura zitagawanywa kati ya Dkt Ruto na Bw Odinga.

Bw Odinga ambaye anaonekana kuungwa mkono na Rais Kenyatta, ameanzisha juhudi za kupunguza umaarufu wa Dkt Ruto katika eneo la Mlima Kenya. Ili kumpiku Dkt Ruto, Bw Odinga atahitajika kuhakikisha amepata zaidi ya asilimia 90 ya kura katika ngome yake ya Nyanza, Magharibi na Pwani; na zaidi ya asilimia 70 maeneo ya Ukambani na Nairobi.

Vilevile, Bw Odinga anayetarajiwa kuzindua kampeni yake rasmi Desemba 9, mwaka huu, atahitajika kumega kiasi kikubwa cha kura katika eneo la Bonde la Ufa, haswa kaunti za Wamaasai, na Kaskazini Mashariki.Eneo la Kaskazini Mashariki linalojumuisha Kaunti za Marsabit, Isiolo, Wajir na Garissa, lina jumla ya wapigakura 820,000.

Eneo la Magharibi linalojumuisha Bungoma, Kakamega, Busia, Vihiga na Trans Nzoia lina jumla ya wapigakura milioni 2.45. Dkt Ruto ana idadi kubwa ya wafuasi katika Kaunti ya Trans Nzoia iliyo mpakani mwa Bonde la Ufa na eneo la Magharibi.

Iwapo kiongozi wa Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi atawania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, huenda akampunguzia kura Bw Odinga kwa kiasi kikubwa.Bw Odinga alishinda Rais Uhuru Kenyatta kwa wingi wa kura katika maeneo ya Nairobi na Pwani kwenye uchaguzi wa 2013 na Agosti 8, 2017. Matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8, 2017 baadaye yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu baada ya kupatikana na dosari.

Katika uchaguzi wa Agosti 8, 2017, Bw Odinga alipata kura 828,826 jijini Nairobi huku Rais Kenyatta akifuatia kwa kura 791,291. Katika Kaunti ya Mombasa na Kilifi Bw Odinga alipata kura 342,337 na 327,831 mtawalia. Rais Kenyatta alipata jumla ya kura 148,765 katika kaunti hizo mbili za kanda ya Pwani.