Connect with us

General News

Magavana 6, wabunge 10 hatarini kutowania – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Magavana 6, wabunge 10 hatarini kutowania – Taifa Leo

Magavana 6, wabunge 10 hatarini kutowania

NA JOSEPH WANGUI

HUENDA wabunge 10 na magavana sita walio uongozini wakazuiwa kuwania nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa Agosti, 9 kwa madai ya ufisadi endapo mahakama ya juu itakubali ombi lililowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtatah.

Bw Omtatah anataka Mahakama iamrishe Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iwazuie viongozi ambao wamehusika na ufisadi na wizi wa mali ya umma kuwania nyadhifa mbalimbali.

Katika ombi lake, Bw Omtatah anadai kwamba hitaji la kisheria ambalo linaashiria kuwa mtu ni mshukiwa hadi anaposhtakiwa na kuthibitishwa kuwa ana hatia halifai kutumika miongoni mwa wanasiasa hasa katika kuwaondoa na kuwazuia kuwania viti mbalimbali vya kisiasa.

Anasema kwamba hitaji hilo linatumika katika kesi za uhalifu na halifai kutumiwa kuzuia IEBC kutekeleza jukumu lake la kukagua na kuwaidhinisha watu wanaogombea viti vya kisiasa.

“Wanasiasa mbalimbali ambao wana rekodi ya ufisadi wanafaa kupigwa msasa na kupata kibali kuwania viti kutoka kwa IEBC. Sheria ya kuwa mtu hana hatia hadi anaposhtakiwa na kupatikana na hatia kortini inafaa tu kutumika kwa wahalifu wengine na sio wanasiasa,” akasema Bw Omtatah.

Anasema kuwa kifungu hicho cha kisheria hakifai kuzuia IEBC kutekeleza wajibu wake.

“Kulingana na sheria mtu anastahili kuchaguliwa kuwa mwanachama wa bunge la kaunti au mbunge ikiwa anatimiza matakwa yote ya elimu, maadili yaliyowekwa na Katiba au na Sheria,” anasema.

Bw Omtatah ana hofu kwamba IEBC itawasafisha wawaniaji ambao hawatatimiza matakwa ya kimaadili yaliyowekwa na Katiba.

Iwapo ombi lake litapitishwa maisha ya kisiasa ya viongozi 16 waliochaguliwa yataathiriwa kwa kuwa wanapaswa kufika mbele ya tume ya kupambana na ufisadi nchini.

Wanasiasa hao ni magavana Anne Waiguru (Kirinyaga), Muthomi Njuki (Tharaka Nithi), Ali Korane (Garissa), Okoth Obado (Migori), Moses Lenolkulal (Samburu) na Sospeter Ojaamong (Busia).

Katika Bunge la Kitaifa, hatua za kisheria zitawaathiri wabunge Jonah Mburu (Lari), Pavel Oimeke (Bonchari), Rigathi Gachagua (Mathira), Aduma Owour (Nyakach), James Gakuya (Embakasi Kaskazini), Ayub Savula (Lugari) na Moses Kuria (Gatundu Kusini).

Wengine ni John Waluke (Sirisia), Alfred Keter (Nandi Hills), Seneta wa Bomet Christopher Langat pamoja na magavana waliotimuliwa Ferdinand Waititu (Kiambu) na Mike Sonko (Nairobi).

Wiki iliyopita Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) katika ripoti yake ilisema kuwa inasubiri amri ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kuwashtaki Bi Waiguru, Bw Kuria na Bw Langat mahakamani.

Bi Waiguru anachunguzwa kwa madai ya kutumia vibaya ofisi.

Ilisemekana kuwa gavana Waiguru alipokea Sh10.6 milioni kwa safari zisizo rasmi. EACC inataka kumshtaki kwa kosa la ufisadi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending