Connect with us

General News

Magavana walipe madeni ya kaunti – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Magavana walipe madeni ya kaunti – Taifa Leo

TAHARIRI: Magavana walipe madeni ya kaunti

KITENGO CHA UHARIRI

RIPOTI ya Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA) iliyotolewa Jumanne inabainisha wazi kuwa magavana 22 wanaohudumu muhula wa pili wataachia raia na warithi wao zigo la Sh31.6 bilioni na wakandarasi hewa kufikia Juni 30, 2021.

Hii ina maana kuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuwa wanakandarasi hao walitoa huduma au bidhaa kwa serikali za kaunti husika.

Magavana wa muhula wa pili watakaoacha mzigo mkubwa wa madeni yanayotiliwa shaka ni kiongozi wa Mombasa Hassan Joho (Sh 1.8 bilioni), Salim Mvurya (Kwale, Sh1.6 bilioni), Cyprian Awiti (Homa Bay, Sh1.4 bilioni) na Josphat Nanok (Turkana) Sh1.1 bilioni).

Wengine ni magavana Martin Wambora (Embu), Sh878 milioni, Paul Chepkwony (Kericho) Sh462 milioni), Patrick Khaemba (Trans Nzoia) Sh414 milioni) na Alfred Mutua (Machakos) Sh344 milioni), Amason Kingi (Kilifi) Sh245 milioni, James Ongwae (Kisii), Sh214 milioni na Ali Roba (Mandera) Sh203 milioni kati ya wengineo.

Magavana wa muhula wa pili walio na kiasi cha chini zaidi cha madeni ya wanakandarasi wanaotiliwa shaka ni Prof Kivutha Kibwana (Makueni, Sh2 milioni), Wycliffe Oparanya (Kakamega, Sh3 milioni).

Uwepo wa kandarasi zinazotiliwa shaka ni changamoto kubwa kwani hiyo ni ishara ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Bunge, Hazina Kuu ya Kitaifa na Ofisi ya Mdhibiti wa Bajeti, zinapaswa kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kandarasi zinatolewa kwa uwazi kuzuia kupotea kwa fedha za umma.

Huwa ni changamoto kubwa kwa gavana mpya anayechukua hatamu za uongozi wa serikali za kaunti pale unapobadilika bila kulipa fedha za kandarasi zinazotiliwa shaka.

Magavana wapya wa Nairobi, Nakuru, Pokot Magharibi, Laikipia, Vihiga, Kitui, Nyandarua, Tana River, Kirinyaga na Kisumu walirithi kutoka kwa watangulizi wao kiasi cha juu cha madeni ya wakandarasi hewa kutoka kwa watangulizi wao baada ya uchaguzi wa 2017.

Magavana wengi waliochaguliwa 2017, wamekataa kulipa madeni hayo yanayotiliwa shaka.

Washinikizwe kulipa madeni haya.

Vilevile, warithi wa magavana watakaokamilisha muhula wa pili mwaka 2022, huenda wakakataa kulipa madeni hayo yanayotiliwa shaka.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending