Connect with us

General News

Magoha aonya watahiniwa na wasimamizi wanaobeba mabunda ya pesa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Magoha aonya watahiniwa na wasimamizi wanaobeba mabunda ya pesa – Taifa Leo

KCSE 2021: Magoha aonya watahiniwa na wasimamizi wanaobeba mabunda ya pesa

NA MWANGI MUIRURI

WAZIRI wa Elimu Prof George Magoha ametoa amri ya kukamatwa mara moja kwa watahiniwa, wasimamizi na walimu watakaonaswa wakiwa na vitita vya pesa mifukoni kipindi hiki ambapo Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) unaendelea.

Prof Magoha amesema kwamba kuna baadhi wanaonaswa wakiwa na maelfu ya pesa mfukoni na udadisi ni kwamba wanalenga kuhujumu uwazi unaohitajika.

“Maafisa wa usalama wanafaa kukamata yeyote ambaye anashiriki zoezi la KCSE akiwa na nia ya kuiba mtihani. Haielezeki ni kwa nini afisa ambaye anaripoti katika kituo cha mtihani kuusimamia lakini mfukoni ana Sh300,000. Ni za nini?” akahoji.

Prof Magoha alikuwa akiongea katika makao makuu ya kaunti ndogo ya Murang’a Kusini aliposhirikisha kusambazwa kwa nakala za mtihani.

Alisema kwamba kwa sasa changamoto ambazo zilikuwa zinakumba shughuli hiyo katika siku za mwanzo zimekabiliwa na hali kulainishwa.

“Tulikuwa na shida ndogo za usambazaji na upakiaji. Tumesuluhisha suala hilo na kwa sasa tumeziba hitilafu hiyo,” akasema.

Ametoa onyo kwa walimu wakuu ambao waneunda njama za kila aina za kuhakikisha kuwa wamepata nakala za ziada za mtihani.

“Wanaagiza nakala za ziada kwa kisingizio cha kuwa na watahiniwa walio na shida za macho. Nakala hizo huwa zimechapishwa kwa hati kubwa. Kuna baadhi wanazitimia kushirikisha njama ya kuiba mtihani kwa kuwa zitasomeka kwa umbali kabla ya kuanza kwa saa mahususi ya kujibu maswali,” akasema.

Prof Magoha amesema kwamba kwa sasa KCSE imekumbwa na visa vitatu pekee vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wasimamizi.

“Ingawa tunajua visa vichache vinaweza vikahujumu shughuli hii yote, tunajaribu sana kuhakikisha madhara yatokanayo na utovu wa maadili yamebakia katika kiwango cha chini,” akasema.

Katika hali hiyo, alionya wote walio katika shughuli hiyo wakijihusisha na mitandao ya kujaribu kufanya udanganyifu wajue hatari ya kukamatwa inawakodolea macho.

“Wewe ikiwa umechukua pesa za wenyewe kwa nia ya kusaidia vitendo vibaya vya wizi wa mtihani wa KCSE ujue tu ni busara urejeshe kwa kuwa uking’ang’ania kufaulu katika njama hiyo utaishia jela,” akasema. 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending