Connect with us

General News

Mahakama ya Rufaa sasa yairuhusu IEBC kutoa zabuni ya karatasi za kura – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mahakama ya Rufaa sasa yairuhusu IEBC kutoa zabuni ya karatasi za kura – Taifa Leo

Mahakama ya Rufaa sasa yairuhusu IEBC kutoa zabuni ya karatasi za kura

NA IBRAHIM ORUKO

HATIMAYE Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inaweza kutoa zabuni ya uchapishaji wa karatasi za kupigia kura na vifaa vya kieletroniki vitakavyotumiwa siku ya uchaguzi mkuu.

Hii ni baada ya Mahakama ya Rufaa kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na kampuni zilizoshindania zabuni hiyo na kuangushwa.

Kampuni hizo zilitaka zabuni za uchapishaji karatasi za kupigia kura na ununuzi wa vifaa vya kieletroniki vya uchaguzi (Kiems) vitakavyotumika katika uchaguzi huo wa Agosti 9.

Majaji Daniel Musinga, Roselyne Nambuye na Fatuma Sichale walisema mahakama hiyo haingeweza kusikiza kesi hiyo kwa kuwa haina mamlaka ya kufanya hivyo. “Baada ya kubaini kuwa hatuma mamlaka ya kisheria kusikiza kesi hii, jambo la busara kwetu kufanya ni kujiondoa,” majaji hao wakasema katika uamuzi uliotolewa Machi 4.

IEBC ilikuwa imetoa zabuni hizo mbili kwa kampuni za kigeni. Lakini kampuni ya Risk Afrika Innovatis Ltd ilielekea kortini kupinga hatua hiyo. Zabuni ya thamani ya Sh3 bilioni ya uchapishaji na uwasilishaji wa karatasi za kupigia kura ilipewa kampuni ya asili ya Ugiriki, Inform P Lykos.

Nayo zabuni ya thamani ya Sh4 bilioni ya uwasilishaji, uwekaji na utunzaji wa vifaa vya Kiems ilipewa kampuni ya Uholanzi kwa jina, Smartmatic.

Vifaa hivyo vya kieletroniki ndivyo vitatumika kuendeshea uchaguzi huo mkuu. Kwanza, kampuni ya Risk Africa ilipinga utoaji wa zabuni ya Kiems kwa kuwasilisha rufaa katika Bodi ya Kusikiza Malalamishi kuhusu Zabuni za Umma (PPARB).

Bodi hiyo ilifutulia mbali utoaji wa zabuni hiyo kwa kampuni ya Smartmatic baada ya kusikiza mawasilisho kutoka pande zote. Bodi hiyo pia iliamuru IEBC kutangaza upya zabuni hiyo ndani ya siku 30 baada ya kutolewa kwa uamuzi huo.

Japo haikushiriki katika vikao vya kusikizwa kwa rufaa hiyo katika PPARB, Smartmatic, ilielekea katika Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa bodi hiyo.

Smartmatic ilisema bodi hiyo ilikiuka mamlaka yake ilipotoa uamuzi huo na kwamba uamuzi wake sasa haukuwa na mantiki na hivyo “ni haramu”.