Katika video hiyo ambayo ilipakiwa kwenye mtandao wa Twitter, mama mmoja na mwanamume ambao wanaonekana kuwa wahudumu wa duka hilo wanaonyeshwa wakiendelea na shughuli zao.
Dakika chache baadaye, wanaume wawili waliokuwa wamejihami wanaingia ndani ya duka hilo huku mmoja akizungumza na wauzaji hao na mwingine anaingia ndani ya duka hilo kupitia kijilango.
Majambazai hao walikuwa wamejihami na bunduki walipowavamia wauzaji hao. Picha: UGC. Source: Depositphotos
Majambazi hao waliwaamuru wauzaji hao wa pombe walale chini katika kona moja ya duka hilo.
Kisha mmoja wao alimsukuma ndani mwanamume mmoja ambaye anaonekana kuwa mteja huku mhalifu mwenzake akikagua duka hilo na kuweka vitu vilivyokuwa ndani ya kabati mfukoni.
Ghafla bin vuu wahalifu hao walikuwa wamemaliza kutekeleza uhalifu wao na kisha wakaondoka kwa duka hilo.
Polisi wameanzisha kuwasaka wawili hao kulingana na ripoti ya Simon Mbugua ambaye ni mwakilishi wa EALA.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.