Connect with us

General News

Makueni sasa kielelezo cha kaunti zenye huduma bora – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Makueni sasa kielelezo cha kaunti zenye huduma bora – Taifa Leo

Makueni sasa kielelezo cha kaunti zenye huduma bora

JAMES MURIMI NA PIUS MAUNDU

BAADHI ya kaunti zimeweka mipango thabiti ya kuhakikisha wakazi wanapata huduma za afya bila kutatizika.

Katika sehemu za kaunti ya Laikipia, serikali ya Gavana Ndiritu Muriithi imeanzisha mpango wa afya wa kaunti hiyo unaofahamika kama Laikipia Health Service (LHS) ambao wakazi wanasema umeanza kuzaa matunda.

Afisa Mkuu wa Afya wa Kaunti hiyo, Dkt Donald Mogoi alisema kwamba, mpango huo utapeleka huduma za afya karibu na raia na kuhakikisha tekinolojia inatumiwa kutoa huduma za afya.

“Jumula ya pesa tu – lizowekeza katika mpango huu ni Sh230 milioni. Kama LHS, tunalenga Afya kwa Wote (UHC),” alisema Dkt Mogoi. Katika kaunti ya Makueni, mpango wa afya kwa wote umedumu kwa miaka mitatu sasa na umeandikisha ufanisi mkubwa.

Hospitali za kaunti hiyo zina dawa na vifaa. Mwishoni mwa mwaka jana, Gavana wa kaunti hiyo Kivutha Kibwana alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Makueni mjini Wote kudhihirisha kaunti yake imepiga hatua kutoa huduma bora kwa wakazi.