Malawi inatarajiwa kurejea debeni Jumanne, Juni 23 miezi mitano baada ya matokeo ya uchaguzi wa urais kufutiliwa mbali na mahakama kuu kwa ajili ya kukumbwa na utata
Viongozi wa upinzani nchini humo walipinga matokeo hayo wakidai yalikubwa na udanganyifu mkubwa na kutaka uchaguzi urudiliwe.
Rais Peter Mutharika ambaye bado yuko madarakani kwa sasa alitangazwa kuwa mshindi mwezi Mei mwaka wa 2019 baada ya kupata ushindi wa asilimia 38.5% kwa jumla ya kura zilizopigwa.
Lakini viongozi wa upinzani walipinga matokeo hayo mahakamani wakidai kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu.
Kwa sasa wapinzani wa chama cha upinzani nchini humo wamemtambulisha mgombea mmoja ambaye atamenyana na Rais Mutharika.
Kwa miezi kadhaa sasa, raia wa Malawi wamekuwa katika mgogoro wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.